ENEO HATARI SANA...

 
Ni ama hawalioni au wanalifumbia macho, lakini ukweli unabaki pale pale kwamba shimo hili kwenye moja ya kona za kuelekea Changanyikeni maeneo ya jirani na Ofisi za Utawala za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ni hatari kuliko inavyodhaniwa. Kwa mujibu wa wenyeji wa maeneo ya Changanyikeni, ajali nyingi za magari zimekuwa zikitokea katika eneo hilo na hadi sasa kusababisha vifo vya watu watatu akiwamo Profesa wa Chuo hicho. Hivi karibuni uongozi wa chuo hicho ulifanya ukarabati wa sehemu ya barabara hiyo kwa kuweka matuta ili kudhibiti ajali zinazotokana na magari kupita kwa kasi na kuhatarisha maisha ya wanafunzi na watumiaji wa barabara hiyo. Lakini cha kushangaza, wajenzi hao waliishia kuweka tuta la mwisho mita kumi kabla kufikia eneo hili hatari. Ttunaweza kusema Uongozi wa chuo haujashuhudia ajali lakini hata kusikia basi vifo hivyo?

No comments: