CHRISTIAN BELLA AJA NA "USILIE"...

 EXCLUSIVE!! Mwanamuziki mkali wa mavoko wa bendi ya Akudo Impact, Prezdaa Christian Bella "Obama" ameachia video ya single yake matata ya Usilie akimshirikisha mkali wa Bongo Fleva, Banana Zorro. 'Combination" hiyo imeweza kuzaa kitu kikali ambacho ziro99blog pekee ndiyo imepewa ruhusa na Prezdaa Bella kuwaletea mashabiki. Video hiyo itarushwa hapa wakati wowote ndani ya blogu hii mwishoni mwa wiki.

ziro99blog inapenda kuwatangazia wanamuziki wote wenye nia ya kujinadi ama kunadi kazi zao kupitia blogu hii bila malipo yoyote kama alivyofungua pazia Prezdaa Bella. Ni rahisi, tuma video yako kwa email yetu ya ziro99blog@gmail.com au piga simu: 0713 477477 au fika ofisini kwetu Kinondoni, Mwanamboka Complex, 2nd Floor. Wote karibuni tuinue muziki wetu! - UONGOZI

No comments: