Tuesday, March 27, 2012

CHEKA TARATIBU...

Mwanafunzi alikuwa darasani kwenye kipindi cha somo la Hesabu. Mwalimu akauliza swali, "Kuna ndege watano kwenye waya wa umeme na wewe ukampiga mmoja kwa manati yako, watabaki wangapi?" Mwanafunzi mmoja akajibu, "Hakuna, maana wote waliobaki wameruka." Mwalimu akasema, "Umekosa, jibu ni wanne. Ila nimependa jinsi ulivyofikiria." Mwanafunzi ikamuuma sana kukosa lile swali ndipo naye hakukubali na hapohapo akamwambia yule mwalimu, "Na mimi nina swali nataka kukuuliza." Mwalimu akajibu, "Sawa, uliza." Mwanafunzi akauliza, "Kuna wanawake watatu wanakula. Mmoja anakula chipsi kuku, mwingine chipsi mayai na wa mwisho chipsi mishikaki. Sasa yupi kati yao ameolewa? Mwalimu akajibu, "Bila shaka aliyekula chipsi mayai!" Mwanafunzi akasema, "Umekosa, jibu ni yule mwenye pete ya ndoa kidoleni. Ila nimependa ulivyofikiria!" Ngoma droo...

No comments: