Mwimbaji Robbie Williams amejitokeza wa kwanza kutaka kununua jumba alimofia mkali wa miondoko ya Pop, Michael Jackson "Wacko Jacko".
Wadaku wamemwona akikagua jumba hilo Alhamisi iliyopita mchana akiwa amefika hapo akiendesha gari lake aina ya Range Rover.
Jumba hilo liliorodheshwa kwenye nyumba zinazouzwa ikianishwa kwa bei ya Dola za Kimarekani milioni 23.9.
Tunajua kila mmoja anayelitaka jumba hili anatakiwa aoneshe kwamba wanaweza kununua kwa bei hii iliyowekwa.
Kama ilivyo kwa Robbie, gazeti moja la London liliwahi kuchapisha taarifa mwaka jana likadiria utajiri wake kufikia Dola milioni 149.
Robbie kwa sasa anamiliki jumba lililoko eneo la Beverly Hills ambalo alinunua mwaka 2008 kwa Dola milioni 16.
Pia aliweza kununua nyumba nyingine mtaani hapo na amekuwa akitumia ardhi hiyo kwa ajili mchezo wa Soka. Kwa sasa huo ni sehemu ya utajiri wake.
Jumba hilo lililoko Holmby Hills, Michael alikuwa amepanga kutoka Hubert Guez, Mkurugenzi Mtendaji wa Ed Hardy. Jumba hilo liko kwenye eneo lenye ukubwa wa Futi za mraba 17,000, lina vyumba 7 na mabafu 13.
Inaonekana Robbie amevutiwa na jumba hilo na kwamba anataka kununua. Lakini Msemaji wa Robbie hakusema chochote kuhusiana na hili.

No comments:
Post a Comment