Saturday, February 18, 2012

WAZO ZURI LILILOSHINDWA

Aliyetoa wazo hili hakika tunampongeza sana hasa kwa kuona umuhimu wa askari wetu wa usalama barabarani kuondokewa na adha ya jua na mvua ili kurahisisha kazi yao. Lakini inaonekana wazo hilo limepokewa kwa namna tofauti na walengwa baada ya vibanda vingi vilivyotapakaa jijini kuwa vitupu kama kilivyokutwa hiki kwenye makutano ya Barabara za Morogoro na Bibi Titi Mohamed eneo la Akiba mchana wa leo. Kama una lolote la kuchangia: ziro99blog@gmail.com

No comments: