WAZIRI MKUU AONGOZA MAMIA KUAGA MIILI AJALI YA PRECISIONAIR

 

Waziri Mkuu, Kassim Majal-iwa ameongoza mamia ya waombolezaji kuaga miili ya watu 19 waliokufa katika ajali ya ndege ya Kampuni ya Precision Air katika Ziwa Victoria mjini Bukoba mkoani Kagera juzi.
Majaliwa aliwaeleza waombolezaji kwe-nye Uwanja wa Michezo wa Kaitaba mjini Bukoba kuwa Rais Samia Suluhu Hassan ameagiza mazishi na maziko ya marehemu hao yagharamiwe na serikali.
Aliwaagiza wakuu wa mikoa katika maeneo husika na kamati za usimamizi wa maafa katika ngazi ya mkoa na halmashauri ambazo wakuu wa wilaya ni wasimamizi wasimamie kikamilifu mazishi hayo.
Alisema ndege hiyo ya abiria yenye uwezo wa kubeba watu 48, ilikuwa na watu 43 wakiwamo abiria 39, marubani wawili na wahudumu wa ndege wawili.
Watu 24 waliokolewa na 19 walipoteza maisha akiwamo rubani na msaidizi wake wa ndege hiyo iliyosajiliwa kwa namba H5W-PW-F aina ya ATR42-500.
Waziri Mkuu alisema wananchi wawili waliokuwa sehemu ya uokoaji walipata madhara na kufikishwa hospitalini na wa-naendelea vizuri.
Alisema ajali hiyo ilitokea saa 2:45 asu-buhi wakati ndege hiyo ikitaka kutua katika Kiwanja cha Ndege cha Bukoba.
Alisema ndege hiyo ilianguka katika Ziwa Victoria mita 500 kutoka katika ki-wanja hicho cha ndege.
“Hali ya hewa katika uwanja wa ndege wa Bukoba ina tabia ya kubadilika na jana (juzi) saa mbili hali ya hewa ilibadilika wakati rubani akiwa hatua za mwisho za kutua kukawa na mvua na upepo na mgan-damizo,” alisema.
Alisema wakati ajali hiyo inatokea kulikuwa na mvua, radi, ukungu kidogo na mgandamizo wa hewa. Alisema Watanzania walipatwa na mshtuko kutokana na ajali hiyo.
Alieleza kuwa ndege hiyo ilitoka Dar es Salaam juzi saa 12:00 asubuhi ikienda Mwanza kupitia Bukoba.
Aliwasilisha salamu za rambirambi kwa wafiwa na waliojeruhiwa katika ajali hiyo kutoka kwa viongozi wa kitaifa akiwamo Rais Samia, Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango na Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi.
Alisema viongozi hao wanaungana na wana Kagera, wafiwa wote na Watanzania kwa ujumla katika kuomboleza msiba huo  mzito kwa taifa na wanaendelea kufuatilia hatua kwa hatua.
Viongozi wengine waliotuma salamu za pole ni Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson na Jaji Mkuu, Profesa Ibrahim Juma.
Majaliwa alisema pia kwa niaba ya Watanzania, Rais Samia amepokea salamu za pole kutoka kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Nigeria, Yemi Osinbajo, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Burundi, Gervais Ndirakobuca na mabalozi wote wa Tanzania katika nchi mbalimbali.
“Kwa sasa timu ya wataalamu inaende-lea, nawasihi wananchi utulivu mpaka timu itakapokamilisha na kutoa taarifa kwa umma itakapokamilisha kazi,” alisema.
Alisema serikali imeunda timu maalumu itakayojumuisha wataalamu kutoka kada mbalimbali ikiwamo Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi ili kuchunguza ajali hiyo.
Alitoa pongezi na shukrani kwa kusaidia katika uokoaji baada ya ajali hiyo kwa uon-gozi wa Mkoa wa Kagera, Kamati za Ulinzi na Usalama za ngazi ya Mkoa na Wilaya, vyombo vya ulinzi na usalama ambavyo ni JWTZ, Polisi, Uhamiaji na Zimamoto.
Pia alishukuru na kuzipongeza taasisi za serikali ikiwamo Skauti, Shirika la Msalaba Mwekundu, watumishi wa kiwanja cha ndege, madaktari, Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wakuu wa mikoa ya Mwanza na Geita.
Kwa sekta binafsi, alitoa shukrani na pongezi kwa Kiwanda cha Sukari Kagera kwa kutoa mitambo, Songoro Marine ya Mwanza, Gereji ya Sabri iliyotoa vifaa, Mgodi wa GGM Geita, Kampuni ya ujenzi wa barabara kutoka Missenyi na wakuu wa mikoa ya Mwanza na Geita.
Pia, aliwapongeza wananchi wa Bukoba na kikundi cha wavuvi kilichojitolea na kutoa msaada wao wa uokoaji.
Aliagiza ofisi ya Waziri Mkuu ambayo ina kitengo kinachoratibu wajasiriamali kwa kumuagiza Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu atoe mafunzo kwa wavuvi na wali-oshuhudia tukio na kushiriki katika uokoaji.
Mkurugenzi Mkuu wa Precision Air, Patrick Mwanri alisema tukio hilo ni kubwa katika historia ya kampuni hiyo na alitoa pole kwa ndugu na jamaa wote waliopoteza ndugu na waliojeruhiwa kutokana na ajali hiyo.
Mwanri alisema rubani kiongozi wa ndege hiyo, Buruhani Rubaga alikuwa mzoefu na mwandamizi katika kazi hiyo na mara nyingi alipenda kuwafundisha wenzake.
“Ni pigo kwetu, taifa na sekta ya anga.
Peter Omondi, rubani msaidizi ni kijana na rubani anayechipukia na alikuwa na mwele-keo mzuri. Hivi karibuni tulimchagua kuwa Ofisa Usalama,” alisema Mwanri.
Alisema wamechukua jukumu la kusafirisha miili hadi kwa ndugu zao baada ya hapo taratibu nyingine zitafuata.

No comments: