KIJANA AKWAA MAMILIONI, AJIRA AJALI YA PRECISION AIR
Rais Samia Suluhu Hassan ameagiza kijana mvuvi aliyesaidia kwa ujasiri kuokoa abiria waliopata ajali ya ndege ya Precision Air, Majaliwa Jackson kukabidhiwa kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni ili atafu-tiwe nafasi kwenye Jeshi la Uokoaji.
“Rais Samia ambaye amekuwa akifuatilia tukio hili, wakati Mkuu wa Mkoa (wa Kagera Albert Chalamila) anaongea na kutoa shukra-ni na pongezi ambazo zote tunamuunga mkono kwamba kijana yule aliyeona ndege kwa mara ya kwanza na kufungua mlango, kwa ujasiri wake huo Rais ameagiza atafu-tiwe nafasi kwenye jeshi la uokozi,” alisema Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
Alisema hiyo itamwezesha kijana huyo aingizwe katika jeshi hilo na kupata mafunzo ya ujasiri zaidi katika uokoaji.
Alisema amefurahishwa na maelekezo ya Rais na baada ya tukio hilo akiwa Mtendaji Mkuu wa Serikali anamuelekeza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi awasiliane na kijana huyo apate taratibu na anuani zake ili aingie kwenye Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
“Nitumie nafasi hii kumshukuru Mheshi-miwa Rais kwa maelekezo yake na nimhakik-ishie kwamba maagizo yake tumeyachukua na tutayatekeleza,” alisisitiza.
Awali, akitoa taarifa ya Mkoa wa Kagera kuhusu ajali hiyo, Mkuu wa mkoa huo, Al-bert Chalamila alimpongeza kijana huyo kwa ujasiri wa kujitolea kuokoa abiria waliokuwa kwenye ndege licha kuwa hajawahi hata siku moja kusogelea ndege.
Katika tukio hilo la kuaga miili ya watu 19 waliofariki, mvuvi huyo Majaliwa alipewa takribani Sh milioni 4.3 na viongozi mbalim-bali kama pongezi.
Chalamila alimkabidhi Sh milioni moja ambayo aliagizwa na Waziri Mkuu Majaliwa ampatie, huku Mbunge wa Bukoba, Steven Byabato akimpatia Sh 300,000.
“Leo nitakupa milioni moja, umefanya kazi kubwa sana ya uokoaji. Naomba tulipo-kee jambo hili kama kudra za Mungu pekee (ajali), kijana huyu mwenyewe anasema hajawahi kuwa hata karibu na ndege, lakini ameokoa wenzake,” alisema Chalamila.
Pia, Kampuni ya Precision Air ilitoa Sh milioni mbili kwa umoja wa vijana walio-saidia uokoaji juzi ndege hiyo ilipoanguka, ambao Majaliwa ni mmoja wa wavuvi hao.
Wakati kijana huyo akipongezwa, aliitwa mbele na mkuu wa mkoa na kumtambulisha kwa wananchi wa Kagera na kisha alisa-limiana na Waziri Mkuu huku wakati wote akibubujikwa na machozi.
Majaliwa ambaye ni mvuvi ni kijana wa kwanza kuiona ndege ya Precision ikianguka na kuwakusanya wavuvi wenzake kwenda kuokoa, ndiye aliyevunja kwa kasia lake mlango wa ndege hiyo na kusaidia abiria kujiokoa.
Taarifa zilizopatikana mapema Leo zinaema kwamba kijana Majaliwa atapelekwa mkoani Tanga kwenda kupatiwa mafunzo kwa meiji minne na kisha Kuba rasmi askari wa Jeshi la Zimamoto spande wa uokoaji.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment