Mwalimu Cox alipokuwa akitoka mahakamani. |
Mwalimu wa kike ambaye alikuwa na
mahusiano ya kimapenzi na mwanafunzi wake wa kiume mwenye umri wa miaka 16
ametahadharishwa kwamba anakabiliwa na adahabu ya kifungo jela baada ya
mahakama kuelezwa kwamba alikuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na mtoto huyo
kwa kipindi cha miezi sita.
Lauren Cox, miaka 27, alikuwa
akifundisha kwenye shule moja kusini mwa London, ndipo alipojitumbukiza katika
mahusiano na kijana huyo, ambaye hakutajwa kwa sababu za kisheria.
Alipandishwa katika Mahakama ya
Croydon, ambako alikiri mashitaka matano yanayohusiana na mahusiano ya
kimapenzi na kijana mwenye umri wa kati ya miaka 13 na 17 wakati akiwa katika
dhamana yake.
Mashitaka hayo ni pamoja na kugusa
kwa dhamira ya kufanya mapenzi mnamo Machi 9 na Machi 16 mwaka jana na pia
kufanya mapenzi kati ya Aprili na Septemba 2015 wakati akiwa na umri wa miaka
26 na kijana huyo akiwa na miaka 16 tu.
Cox alikamatwa Septemba 16, 2015
baada ya wanafunzi kuwaeleza wazazi wake kuhusu kilichokuwa kikiendelea kati ya
wawili hao.
Kisha baadaye wakawasiliana na
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, ambaye aliwasiliana moja kwa moja na Ustawi wa
Jamii.
Cox alikutana kwa mara ya kwanza na
kijana huyo wakati akiwa na miaka 13, na mwathirika huyo alisema wakaunda
mahusiano ya karibu.
Kwa mujibu wa polisi, mwalimu huyo
akaanza mahusiano ya kimapenzi na kijana huyo mnamo Januari 2015.
Mwendesha Mashitaka Brian Reece,
aliieleza mahakama hiyo; “Tofauti ya umri ni miaka 10 pekee hivyo hii ni
mahusiano ya mwalimu na mwanafunzi.”
Cox na kijana huyo walikuwa wakikutana
baada ya muda wa masomo na wakati wa likizo. Mwalimu huyo alikuwa akimtumia
picha za kimahaba na video alizojirekodi mwenyewe na kumtumia kijana huyo.
Lakini kijana huyo alisitisha
mahusiano hayo Agosti 2015 baada ya wazazi wake kutilia mashaka kilichokuwa
kikiendelea na kumkabili kijana wao ambaye alikiri kuwa na mahusiano na Cox.
Hatahivyo, Cox aliendelea kumtumia
kijana huyo meseji zilizowafanya wazazi wa kijana huyo kuripoti kwa vyombo
husika.
Cox, mwalimu wa masomo ya biashara,
ambaye aliwasili mahakamani hapo akiwa amevalia suruali nyeusi, koti, na miwani
alinyamaza kimya kizimbani wakati akisomewa mashitaka yote matano anayokabiliwa
nayo.
Cox, mkazi wa Oxted mjini Surrey,
alipatiwa dhamana na anatarajiwa kurejea mahakamani hapo mwezi ujao kwa ajili
ya hukumu.
Alipatia dhamana hiyo kwa masharti
ya kutoonana na kijana huyo au kufika shuleni hapo.
No comments:
Post a Comment