Mtoto aliyekuwa na
uvimbe unaoonekana kama kichwa cha pili amenusurika kifo katika upasuaji wenye
hatari kubwa uliodumu kwa masaa sita kuondoa uvimbe huo mkubwa, ambao madaktari
awali walisema hauwezi kutibika.
Yamanoor Naranal,
ambaye ana umri wa miezi mitano tu, alizaliwa nchini India akiwa na matatizo
hayo – hali inayotokea kwa nadra mno ambapo majimaji ya ubongo yanatiririka nje
ya fuvu la kichwa.
Wazazi Karriappa
Naranal, miaka 35, na mkewe Shridevi Naranal, miaka 28, kutoka kijiji cha Tavariyara,
kilichopo jimbo lililoko kusini kwa Karnataka, walielezwa kwamba hakuna
matarajio ya kutibika muda mfupi baada ya mtoto wao kuzaliwa.
Wanandoa hao
waliochanganyikiwa walifika kwenye hospitali hiyo ya serikali mara kadhaa
wakijaribu kutafuta msaada, lakini baada kuwa wameshakata tama ya mtoto wao
huyo wa kiume kuweza kupatiwa matibabu.
Pale mhudumu wa afya
akashauri wazazi hao kumpeleka Yamanoor kwenye hospitali bora zaidi mjini
Bangalore wazaiz hao wakaitumia fursa hiyo – ambayo ilipelekea uondoshwaji wa
uvimbe huo kimiujiza kufuatia upasuaji hatari.
Mr Naranal, ambaye
anafanya kazi kama kibarua wa ujenzi na kulipwa takribani Dola 2 za Kimarekani
(Karibu Shilingi 5,000 za Kitanzania) kwa siku, alisema: “Madaktari wengi
walinieleza kulikuwa na asilimia 90 za mtoto wangu kufa endapo angefanyiwa
upasuaji. Madaktari walisema sikutakiwa kuhatarisha sababu upasuaji wa
mafanikio hautowezekana.
“Lakini tukapata
mwanga wa matumaini mjini Bangalore pale daktari mmoja aliposema kuna nafasi ya
asilimia 50 ya kupona ndipo tukakubali ifanyike.”
Yamanoor akatibiwa
katika Hospitali ya Sapthagiri, mjini Bangalore, mwezi uliopita, na baada ya upasuaji
uliochukua masaa sita madaktari wakaondosha kwa mafanikio uvimbe huo, ambao
ulikuwa na ukubwa wa takribani mzingo wa kipenyo cha sentimeta 20.
Dk Hariprakash
Chakravarthy, bingwa wa upasuaji katika hospitali hiyo, alisema: “Hali hii
hutokea kwa mama ambao wana upungufu wa asidi ya foliki.
“Tatizo hili
hufaamika kama occipital encephalocele,
na hutokea pale kunapokuwa na uwazi kati ya mifupa miwili ya fuvu, na fuvu
linapoendelea unaendelea na kuwa uvimbe uliojaa kimiminika.
“Tulikuwa na
matarijio finyu mno kuhusu kufanikiwa kwa upasuaji huu kuzingatia ukweli kwamba
mtoto mdogo hawezi kumudu kupoteza kiasi kikubwa cha damu.
“Hata upotevu wa mililita
10 hadi 20 za damu unaweza kusababisha moyo kusimama kufanya kazi. Tunapokata
sehemu ya ubongo husababisha upotevu wa kiasi fulani cha damu lakini
tunashukuru hakuna chochote kibaya kilichotokea na mtoto huyu mdogo yu hai.”
Mtoto huyo wa kiume
aliruhusiwa kutoka hospitalini mwishoni mwa wiki iliyopita – takribani mwezi
mmoja baada ya matibabu yake – na sasa anaendelea kujiuguza nyumbani.
Lakini atatakiwa
kufanyiwa upasuaji mwingine mwezi ujao na kufanyiwa uangalizi wa mara kwa mara,
kila baada ya miezi mitatu.
Bw Naranal
aliwashukuru madaktari kwa kumfanyia upasuaji mtoto wake na kusema: “Sasa
anaendelea vizuri, namshukuru sana yule mhudumu wa afya. Mtoto wangu atatakiwa
kuangaliwa afya yake kila baada ya miezi mitatu lakini yote ni heri.
“Siwezi kuamini
simulizi yake ina mwisho wenye furaha. Ninamshukuru Mungu na madaktari hawa.”
3 comments:
Make your profile as appealing as you can, use catchy phrases and prevent being boring.
These scammers usually have only one picture inside their profile, thus it will be the norm for some experienced individuals who date online to feel that one
picture profiles don't show the genuine
person. The choice is yours, do you want to share your existing current email address,
your cell phone numbers, your address and even your surname.
whoah this weblog is great i like studying your articles.
Stay up the great work! You recognize, many people are looking around for this information,
you can help them greatly.
Asking photographer for a picture update? A little over a
week ago my boyfriend and I had an anniversary shoot with a photographer ( had an amazing time).
The day after our session she sent me one sneak peak picture,
which looked amazing! When I asked for an estimate time frame on when we would be getting our photos she told me it usually takes her less...
show more Wait the 2 weeks. If you text before that,
you'll come across as pushy and photographers
don't like that. Sometimes they push your shoot
to the bottom of the list if you appear too pushy.
Post a Comment