Serikali imekataa viwango vya nauli mpya
vilivyopendekezwa na Kampuni ya Uda Rapid Transit (UDA-RT), itakayotoa huduma
ya usafiri wa mabasi yaendayo haraka Dar es Salaam.
Pamoja
na kukataa imeweka bayana kuwa viwango hivyo viko juu ambavyo wananchi wengi
watashindwa kuvimudu.
Kauli
hiyo ya serikali imetolewa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ambaye pia ameagiza
wizara zote zinazohusika kukutana haraka iwezekanavyo na kujadili viwango vipya
vya nauli vinavyoendana na hali halisi ya maisha ya wananchi.
“…
sasa nataka mamlaka zote zilizohusika wakutane na kuja na viwango vipya vya
nauli kama huyu mwekezaji ameshindwa aseme, Serikali inaweza kuendesha mradi
yenyewe,” alisisitiza Majaliwa.
Wizara
na taasisi zilizoagizwa kukutana ni Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa (Tamisemi); Wizara ya Ujenzi na ya Uchukuzi; Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu
na Majini (Sumatra) pamoja na kampuni ya UDA-RT.
Akizungumza
na waandishi wa habari Dar es Salaam muda mfupi baada ya kurejea akitokea
Ruvuma, alikokamilisha ziara yake ya kikazi jana, alisema viwango hivyo vilivyopendekezwa na
vinavyotarajiwa kujadiliwa na Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini
(Sumatra) havifai na havikubaliki.
Alisema
Novemba 25, mwaka jana alitembelea mradi huo wa DART na kumuagiza Katibu Mkuu
wa Tamisemi, Mtendaji Mkuu wa DART pamoja na Wakala wa Barabara (Tanroads)
kupitia mfumo mzima wa uendeshaji wa
mradi huo, lakini hadi leo hakuna mpango wowote wa biashara uliowasilishwa serikalini
na UDA-RT.
Alisema
pamoja na hayo, pia kampuni hiyo imeshindwa kuweka bayana gharama za uendeshaji
wa mradi huo, uliotakiwa kuanza rasmi Januari 10, mwaka huu.
Majaliwa
alisema wakati kampuni hiyo ikishindwa kuweka wazi mpango wake wa kibiashara, alishangaa
juzi kusikia imewasilisha viwango vya nauli vilivyopendekeza ambavyo vilikuwa
vya gharama ya juu.
“Kwa
kukosekana tu gharama halisi za uendeshaji mradi, ni dhahiri kuwa nauli
zilizopendekezwa hazina uhalisia,” alisema.
Kampuni
hiyo ilipendekeza safari kwenye njia kuu kuwa Sh 1,200 na safari katika njia
kuu na pembeni kuwa Sh 1,400 na wanafunzi nusu ya nauli hizo.
“Gharama
hizi ni kubwa mno. Mradi huu unalenga kumlinda na kumsaidia mwananchi wa
kawaida, wakiwemo watumishi wa umma ambao wengi wao wamejenga pembezoni mwa mji
kuweza kusafiri kutoka maeneo ya pembeni hadi katikati ya jiji kwa gharama
nafuu na kwa urahisi na si kumkandamiza,” alisema Majaliwa.
Alisema
kipato cha wananchi kwa ujumla wakiwemo watumishi wa umma, bado si kikubwa.
Alitoa mfano kwamba, mtumishi anayelipwa mshahara wa Sh 250,000 kwa mwezi, kwa nauli
iliyopendekezwa pamoja na watoto wake, fedha yote inaishia kwenye nauli.
Alisema
kwa hali ilivyo, Serikali haiwezi kuridhia viwango hivyo ambavyo ni wazi
vitamkandamiza mwananchi badala ya kumsaidia.
“Bado
tunayo nafasi ya kuendesha mradi huu, si lazima tuanze Januari 10 kama
ilivyopangwa, ni bora tuchelewe na kuanza tukiwa na viwango vya nauli
vinavyoridhisha badala ya kuanza na nauli hizi ambazo ni gharama kubwa mno.”
Juzi
Sumatra ilikutana na wadau kwa ajili ya kujadili mapendekezo hayo ya nauli,
ambayo hata hivyo yalipingwa na wadau wengi wa sekta ya usafiri. Walishauri
nauli iwe kati ya Sh 400 na Sh 500 kutimiza malengo ya kusaidia wananchi wa
kipato cha kawaida.
Pamoja
na hayo wadau hao wakiwemo wananchi na Baraza la Walaji la Sumatra (Sumatra
CCC), walihoji sababu za mabasi hayo yanayobeba watu wengi kwa safari moja na
yanayotumia barabara zisizo na foleni, yatoze nauli kubwa wakati daladala
zinazochukua abiria wachache na kukabiliwa na msongamano mkubwa katika barabara
za kawaida, wanatoza nauli za chini.
3 comments:
I am really glad to glance at this blog posts which consists of lots of useful information, thanks for providing these statistics.
Make your profile as appealing as is possible, use catchy
phrases and prevent being boring. There are many Americans who think that Inter racial relationships needs to be banned because it destroys the
cultures of two races plus brings problem for their siblings.
Meeting web dating is tricky when you are
honest makes it much easier.
Wow, this piece of writing is good, my younger sister is analyzing these
kinds of things, so I am going to tell her.
Post a Comment