Watu watano wamekufa
papo hapo na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya basi la Kampuni ya DON’T WORRY
kugonga Treni ya mizigo katika makutano reli na barabara kuu katika eneo la Malolo, nje kidogo ya mji wa Tabora.
Ajali
hiyo imetokea majira ya saa nane mchana wakati basi hilo lilipokuwa likipita
katika makutano ya Barabara Kuu ya Tabora-Kigoma na Reli ya Kati
(Tabora na Kigoma).
Kwa
mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo dereva wa basi la DON’T WORRY alikuwa katika
mwendo kasi kabla ya kugundua kuna treni inakuja na hivyo kuamua kukwepesha
gari pembeni lakini likamshinda na kupinduka katikati ya barabara ndipo ajali
hiyo ikatokea.
Baada ya ajali hiyo, dereva
huyo akatoroka katika eneo la tukio huku majeruhi na marehemu
wakipelekwa hospitalini.
Wawakilishi
wa Shirika la Reli nchini (TRL) wamewakumbusha madereva kuwa waangalifu na alama
za barabarani ili kuepusha ajali.
No comments:
Post a Comment