Wafungwa wengi
hawapewi haki zao za msingi miongoni mwake, ikiwa ni kukaa muda mrefu
magerezani na mahabusu bila kuonana na ndugu zao.
Aidha Tume ya
Haki za Binadamu na Utawala Bora imetaja polisi kuwa chanzo cha uvunjaji wa
sheria kwa kukamata wahalifu bila
kujitambulisha na pia kutumia
nguvu wanapochukua maelezo kwa mtuhumiwa.
Katibu Mtendaji
wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala bora, Mary Massay aliyasema hayo jana
Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kimataifa unaojulikana kama
‘Luanda Guideline’ kupitisha muongozo wa sheria zilizoandaliwa nchini Angola.
Massay alisema
Tume ilitembelea katika mahabusu na magereza ya nchini walitambua kuwa wafungwa
wengi wamekaa gerezani bila ya kuonana na ndugu zao pamoja na kwamba wanahaki
hiyo.
Kwa mujibu wa
Massay, mkutano huo ulihusisha nchi tano za Afrika, huku wahusika kutoka jeshi
la polisi na magereza hawakufika katika mkutano huo licha ya kwamba walitakiwa
kuhudhuria.
Kamishna kutoka
Tume ya Haki za Binadamu Afrika, Med Kaggwa alisema kumekuwa na tatizo kubwa
katika ufuatiliaji wa haki za wafungwa
na mahabusu.
Ilielezwa
asilimia 50 ya wafungwa waliopo katika magereza nchini, kesi zao zimechukua miaka mitatu hadi minne kuisha.
No comments:
Post a Comment