Mamlaka ya
Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imesisitiza vitambulisho vya uraia,
havitatumika kupiga kura katika uchaguzi
mkuu, isipokuwa kadi
zitakazotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Mkurugenzi
wa Uchaguzi, Julius Mallaba alifafanua
jana jijini Dar es Salaam kwamba ni makosa kudhani kuwa
vitambulisho vinavyotolewa na Nida, vinaweza kutumika kupiga kura.
“Haiwezekani
kabisa…tunaomba watu waelewe kuwa kadi za kupiga kura na vitambulisho vya uraia
ni vitu viwili tofauti. Vitambulisho vya taifa siyo mbadala wa kadi za kupiga
kura,” alisisitiza.
Kwa mujibu
wa mkurugenzi huyo, kwa hali ilivyo utoaji wa vitambulisho vya taifa kwa nchi
nzima, utachukua muda mrefu na kwamba hata baada ya uchaguzi ulioagizwa
kisheria kupita, watu wengi watakuwa hawajapata vitambulisho hivyo.
Mkurugenzi
alitoa ufafanuzi huo, kutokana na kile alichosema ni kutokana na kuwepo taarifa
katika baadhi ya vyombo vya habari kwamba mtu asiye na kadi ya kupiga kura, anaweza kutumia kitambulisho
cha uraia kupiga kura.
Alisema
wakati uandikishaji wa NEC unafanyika kwa muda maalum ili kuwahi upigaji wa
kura ya maoni na uchaguzi mkuu, uandikishaji wa Nida hauna muda maalumu.
“NEC ina
mchakato mfupi wa ukusanyaji wa taarifa za watu wanaoandikishwa na kadi za
mpiga kura zinatolewa papo hapo kituoni baada ya ujazaji wa fomu,” alisema.
Kwa upande
wa Nida, mchakato wa ukusanyaji wa taarifa una utaratibu mrefu kutokana na
wahusika wa zoezi hilo kuwa wengi.
Akielezea
zaidi alisema namba ya kadi inayotolewa na tume ya taifa ya uchaguzi ni ya
kipekee kwa mtu anayeandikishwa.
Nida
inaweza kutoa namba zaidi ya moja endapo itabidi kutoa kitambulisho kingine kwa
mtu huyo huyo, kutokana na kitambulisho cha awali kupotea au kuharibika.
Mallaba
alisema hata kama vitambulisho vya uraia vingekuwa tayari, bado tume ingetakiwa
kuandaa daftari kwa kuwa vitambulisho vya uraia huwa haviainishi mtu ni mpiga
kura wa eneo gani.
Alifafanua
kuwa kama wananchi wote wangekuwa na
vitambulisho vya taifa, kitu ambacho kingefanyika ni kwa tume kununua kifaa
kinachoweza kusoma kitambulisho na kupata taarifa za mhusika na kumpangia
mhusika sehemu yake ya kupigia kura.
Alisema
hakuna nchi katika bara la Afrika,
inayotumia kitambulisho cha taifa moja kwa moja katika kupiga kura, isipokuwa
hutumika kurahisisha utaratibu wa kuandaa daftari la kudumu la wapiga kura.
Kwa upande
wake, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji mstaafu Damian Lubuva
alisema uandikishaji wa vitambulisho vya taifa kwa upande mmoja na vitambulisho
vya wapiga kura kwa upande mwingine ni shughuli
tofauti, lakini zinazohusiana kwa
karibu na pia zinazohusu wananchi.
1 comment:
Naomba niandike kwa sababu nataka kutumia picha ya kadi kwa website yetu. Nitume eMail na oliver.reimer@journafrica.de
Post a Comment