Mfanyakaziwa Benki ya NMB Tawi la Songea,
alinusurika kufa na familia yake jana baada ya nyumba waliyohamia kwa muda,
nayo kuteketea kwa moto.
Tukio hilo limekuja siku nne zilizopita ambapo
akiwa na familia yake, walinusurika kufa baada ya nyumba waliyokuwa wakiishi
kuteketea kwa moto.
Akizungumza namwandishi ofisini kwake, juzi,
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Mihayo Misikela alisema tukio hilo ni la
Agosti 15, mwaka huu saa 5:30 asubuhi katika eneo la Msamala Manispaa ya
Songea.
Kamanda alisema inadaiwa siku hiyo ya tukio,
nyumba ya Maulid Mbaraka iliyopo Msamala ghafla iliungua moto, ulioanzia katika
chumba kimoja kilichokuwa na vyombo mbalimbali vya Hamza Namahala na kuteketeza
mali zote zilizokuwamo na thamani yake haijafahamika.
Alisema inadaiwa moto huo uligunduliwa na
mtoto, Kausar Namahala (12) mwanafunzi wa shule ya mzingi Mfaranyaki, ambaye ni
mdogo wa Hamza Namahala.
Mtoto huyo baada ya kugundua moto huo, ghafla alitoa taarifa kwa majirani ambao
walifika kutoa msaada. Lakini, baadaye walilazimika kutoa taarifa polisi kwa
kikosi cha zima moto na walipofika eneo la tukio, walifanikiwa kuuzima licha ya
kuwa baadhi ya mali zilikuwa zimeshateketea.
Kamanda
Misikela alisema Namahala alipewa vyumba viwili na mfanyakazi mwenzake,
Selemani Mkongo atumie kwa muda kwa kujihifadhi na familia yake baada nyumba
aliyokuwa anaishi kuungua moto Agosti 12 mwaka huu. Katika tukio hilo la Agosti
12, watu watatu wa familia hiyo walizimia na kulazwa hospitali ya Mkoa kwa
matibabu.
No comments:
Post a Comment