Katibu Mkuu wa
Chama cha Maalbino (TAS), Zakia Nsemo
ameiomba Serikali iongeze ulinzi kwa watu wenye ulemavu wa ngozi kutokana na
maisha yao kuwa hatarini.
Nsemo aliyasema
hayo wakati akizungumza jijini Dar es Salaam juu ya vitendo vya kinyama
vilivyoripotiwa kufanyiwa watu wenye ulemavu wa ngozi mkoani Tabora na Simiyu
ambako watu wasiojulikana waliwakata baadhi ya viungo vyao na kutokomea navyo
na mwingine kuuawa.
Alisema vitendo
hivyo vimeanza kushika kasi tena kama ilivyokuwa kipindi kilichopita hali
inayowafanya albino washindwe kufanya shughuli zao zinazowapatia riziki huku
watoto wenye ulemavu wa ngozi pia wakishindwa kwenda shule.
Hivi
karibuni Susan Mungi (35) ambaye ni
albino mkazi wa kijiji cha Buhelele kata ya Nsimbo wilayani Igunga, alikatwa
kiwiko cha mkono wake na wahusika kutoweka nacho.
Katika tukio
hilo, mume wa Suzan, Mapambo Mashili aliuawa kikatili kwa kupigwa na kitu
chenye ncha kali kifuani na kichwani wakati akijaribu kumnusuru mkewe asikatwe
mkono wake.
Tukio hilo
limekuwepo wiki moja baada ya mtoto Upendo Sengerema (15) mkazi wa kijiji cha
Usinge kata ya Uganza wilayani Kaliua mkoani Tabora kukatwa mkono na wahalifu
ambao walikimbia.
No comments:
Post a Comment