Mwanamke
mkazi wa kijiji cha Tuombemungu Kata ya Ugunga wilaya ya Kaliua mkoani Tabora, Mawazo Saidi, ameuawa
kikatili.
Mume
wa mwanamke huyo anatuhumiwa kufanya mauaji hayo, kwa madai ya kudaiwa fedha za
tumbaku.
Mawazo
aliuawa baada ya kutokea ugomvi kati yake na mumewe, unaodaiwa kusababishwa na
fedha za mauzo ya tumbaku.
Mwenyekiti
wa kijiji cha Tuombemungu, Abdulrahman
Anthony alisema tukio hilo ni la saa 6 usiku wa Agosti 15 mwaka huu.
Inadaiwa
kuwa Ally Jinasa, ambaye ni mume wa mwanamke huyo, alirudi nyumbani
akitokea katika kilabu cha pombe na kuanza kubishana na mkewe kuhusu fedha za
tumbaku, ambazo mkewe alitaka kufahamu zilikokwenda.
Inadaiwa
mwanamke huyo alijaribu kumsihi mumewe, kuachana na pombe kwani inarudisha
nyuma maendeleo ya familia.
Pia,
inadaiwa alimtaka aache kuuza tumbaku kwa walanguzi, badala yake aiuze kwenye
chama cha msingi ili fedha
zitakazopatikana, zisomeshe mtoto wao shule.
Inadaiwa
kuwa mume, Jinasa, alipinga ushauri huo na kisha kumkata mkewe huyo kwa panga
kichwani na shingoni na kusababisha ubongo kusambaa. Alifariki dunia wakati
akipelekwa hospitali kwa matibabu.
Kamanda
wa Polisi wa Mkoa wa Tabora, Suzan Kaganda (pichani) akizungumzia tukio alisema mtuhumiwa ametiwa mbaroni na atafikishwa mhakamani muda wowote upelelezi
utakapomilika.
No comments:
Post a Comment