Kampuni
ya Huawei Technologies (T) Limited imeingiza katika soko la nchini teknolojia
mpya ijulikanayo kama ‘enhanced LTE’, (eLTE) itakayopiga jeki serikali katika
vita dhidi ya ujangili nchini.
Akizungumza
wakati wa mkutano uliojumuisha watu waishio ughaibuni uliofanyika jijini Dar es
Salaam hivi karibuni, Meneja Uhusiano wa Huawei, Moses Hella alisema kifaa hicho kitawezesha
kuleta mrejesho wa haraka wa mawasiliano katika nyakati muhimu.
Alisema
kifaa hicho chenye uwezo wa kutuma video kwa haraka, kinaweza kuleta ufanisi
mkubwa katika kampeni zinazoendelea nchini dhidi ya ujangili.
"Tumeleta
katika soko la Tanzania teknolojia mpya iitwayo 'enhanced LTE' ambayo ni
teknolojia ya mawasiliano ya kipekee. Hii ni muhimu hususani kwa ajili ya
mawasiliano muhimu, inayowezesha utumaji wa habari kupitia video, ambayo
hutumika hasa katika usafirishaji wa bidhaa muhimu au watu.
"Kwa
kufunga kamera zisizo na nyaya na kupeleka mfumo wa simu wa ufuatiliaji katika
hifadhi mbali mbali za taifa, kwa kiasi kikubwa itasaidia serikali katika vita
dhidi ya ujangili," alisema Hella.
No comments:
Post a Comment