Mwenyekitiwa Chama Cha
Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete jana alifungua kikao maalumu cha Kamati
Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya chama hicho, ambapo pamoja na mambo
mengine kitajadili mwenendo wa Bunge Maalumu la Katiba.
Akifungua kikao
hicho jana, Rais Kikwete alisema hana ajenda za kikao hicho mfukoni, lakini
wamekutana kwa lengo la kuzungumza mambo yanayoendelea.
“Sina ajenda
mfukoni tumekutana tuzungumze mambo yetu,” alisema na kufafanua kuwa mara ya
mwisho kukutana ilikuwa Julai na safari hii wamekutana ili kuangalia mambo ya
chama yanavyoendelea, na kufanya uamuzi
ili waendelee mbele.
Awali Katibu Mkuu
wa CCM, Abdulrahman Kinana alisema kikao hicho ni maalumu na mpaka
kinafunguliwa jana, wajumbe 33 kati ya 34 walikuwa ukumbini na mjumbe ambaye
hakuweza kufika alikuwa, Jerry Silaa.
Akizungumza na
waandishi wa habari kabla ya kufunguliwa kwa kikao hicho, Katibu NEC wa Itikadi
na Uenezi, Nnape Nnauye, alisema moja ya ajenda katika kikao hicho ni kujadili
mchakato mzima wa Bunge Maalumu la Katiba linaloendelea.
Pia alitoa mwito
kwa waandishi wa habari kuandika habari kutoka chombo husika na sio kuokota
taarifa barabarani na kuonya kuwa atakayekiuka hilo atachukuliwa hatua.
Alisema taarifa
nyingi zinazoandikwa kwenye magazeti si za kweli na kuwataka waandishi kutafuta
ufafanuzi na si kufikiria tu kufanya biashara ya kuuza magazeti. “Tusifanye
biashara na maisha ya nchi,” alisema Nape.
No comments:
Post a Comment