Benki
ya Posta Tanzania kwa kushirikiana na Mfuko wa Pensheni wa LAPF, wamezindua
mpango maalumu wa kutoa mikopo kwa wastaafu.
Akizungumza
katika uzinduzi huo jana jijini Dar es Salaam, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya
Posta, Sabasaba Moshingi alisema wameamua kuanzisha aina hiyo ya mkopo baada ya
kugundua kwamba wastaafu wamekuwa wakipata taabu kupata mikopo kutoka kwenye
taasisi nyingi za kifedha hapa nchini.
“Mkopo
huu ni wa kwanza wa aina yake katika soko la benki hapa nchini na tunaamini
utampa amani mwanachama wa LAPF ambaye amestaafu na utamwezesha kuanzisha ama
kuendeleza biashara yake aweze kutimiza
malengo yake na kujiongezea kipato na hivyo kuondokana na utegemezi wa ndugu au
watoto,” alisema.
Alisema
mstaafu anayetaka kukopa hahitaji kuwa na dhamana, na riba inayotozwa kwa mkopo
huo ni ndogo ukilinganisha na mikopo mingine ambayo ni asilimia 12 kwa mwaka.
Alisema
mkopo umewekewa bima, hivyo endapo mkopaji atafariki familia yake haitaendelea
kudaiwa.
Akizindua
mpango huo, Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka alisisitiza wastaafu
wenye sifa za kuomba mikopo hiyo, kujitokeza kwa wingi na kutumia fursa
hiyo waweze kujiendeleza kimaisha, kwani
wakiitumia vizuri mikopo hiyo itakuwa chachu ya maendeleo yao na kuishi maisha
ya faraja.
No comments:
Post a Comment