Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa raia wawili wenye asili ya bara la Asia
walikiri kupanga njama za kuwateka watoto wawili kwa lengo la kujipatia Sh
milioni 300.
Mawakili
wa Serikali, Mwanaamina Kombakono na Janetoreza Kitali walidai hayo jana mbele
ya Hakimu Mkazi Devotha Kisoka wakati wakiwasomea washitakiwa hao maelezo ya
awali.
Washitakiwa
hao wanaokabiliwa na kesi ya kupanga njama za kuwateka watoto wawili wa Anali
Akber Haji kwa lengo la kujipatia fedha hizo ni Adil Arshad Yusuph (24) na
Mehul Kava (24).
Wakisoma
maelezo ya awali, mawakili hao walidai Machi 16 mwaka jana katika eneo
lisilofahamika, washitakiwa walikubaliana kutekeleza mpango wa kuwateka watoto
hao.
Iliendelea
kudai kuwa katika kutekeleza mpango huo, washitakiwa walikodi watu kwa ajili ya
kuwatekea watoto hao.
Hata
hivyo, hawakufanikiwa baada ya polisi kupata taarifa na kuandaa mtego wa
kuwakamata. Kesi hiyo itaanza kusikilizwa Septemba Mosi mwaka huu.
No comments:
Post a Comment