Wakazi watatu wa kijiji cha Uhelela wilaya ya Bahi, mkoani Dodoma wamekana shtaka linalowakabili la mauaji ya kukusudia ya mama yao mzazi, ambapo wanadaiwa kumshambulia kutokana na kitendo chake cha kumlazimisha mjukuu wake kula mchele.
Washtakiwa katika kesi hiyo ni Mantonya Mdemwa, Mlugu Mdemwa, Mpangwe Mdemwa ambao ni watoto wa marehemu na Mwaja Mgongwe ambaye ni Mjukuu wa marehemu.
Kesi hiyo inasikilizwa na Jaji Moses Mzuna wa Mahakama Kuu Tanzania Kanda ya Dodoma ambapo mama aliyeuawa ametajwa kuwa ni Mnyekulu Mlugu.
Washtakiwa walikuwa wakisomewa mashtaka yao na Wakili wa Serikali Morice Sarara, aliyeiambia Mahakama kuwa Machi 9, mwaka 2009, katika kijiji cha Uhelela baada ya washtakiwa kuhisi mama yao anajihusisha na vitendo vya kishirikina walimshambulia na kumuua.
Alidai siku moja kabla ya kifo chake mjukuu wa marehemu aliyejulikana kwa jina la Antonia ambaye ni mtoto wa mshtakiwa wa kwanza alitoa taarifa kuwa kwa nyakati mbili tofauti marehemu alikuwa akimlazimisha kula mchele na alimuonya kuwa atakufa endapo atatoa taarifa hizo.
Ilidaiwa kuwa baada ya mshtakiwa wa kwanza kupata taarifa hizo alikasirika na kuamua kuwaita kaka zake pamoja na mshtakiwa wa nne ambaye ni mjukuu wa marehemu, na kwenda nyumbani kwa marehemu na walipofika walimhoji kwa nini alikuwa akilazimisha mjukuu wake kula mchele
Sarara alidai mahojiano hayo yalisababisha majirani kufika kwenye mji wa marehemu na washtakiwa waliamua kupeleka suala hilo kwenye uongozi wa kijiji kwa usuluhishi, lakini walipofika njiani mshtakiwa wa pili alimfunga mikono marehemu na washtakiwa kwa pamoja walianza kumshambulia katika sehemu mbalimbali za mwili wake wakitumia silaha za jadi marungu na fimbo.
Baada ya kumshambulia mama yao alikufa na washtakiwa walikimbia eneo hilo na kuacha hapo hapo mwili wa marehemu ambapo uchunguzi wa daktari ulionesha marehemu alikufa kutokana na kipigo kikali hasa upande wa kulia wa ubavu wake.
Washtakiwa walikamtwa kwa nyakati tofauti na kufikishwa polisi kisha mahakamani.
Upande wa mashtaka unatarajia kuita mashahidi 12 kuthibitisha shtaka hilo na upande wa utetezi utaita mashahidi watano.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi hapo itakapopangwa kwenye kikao kingine cha Mahakama Kuu.

No comments:
Post a Comment