Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchini imesema kuna wahalifu 1,694 wa vifungo vya nje, ambao wanaoendelea kutumikia adhabu zao katika taasisi mbalimbali za umma katika mikoa 18 nchini hadi kufikia Juni mwaka huu.
Mkurugenzi Idara ya Huduma kwa Jamii, Fidelis Mboya alisema hayo Dar es Salaam katika mahojiano maalumu na mwandishi.
Alisema kati ya hao, wahalifu kwa huduma za jamii ni 1,600 ambapo wanawake ni 286. Pia wamo wahalifu wa probesheni ambao idadi yao ni 94, kati yao wanawake wakiwa 21.
Kazi ambazo wahalifu hao wanafanya ni kuchimba mitaro ya maji machafu, kutunza bustani, kufyatua matofali ya kujenga shule na zahanati, kuchimba mashimo ya vyoo, kuandaa, kutunza vitalu vya miche na usafi wa mazingira.
Aidha, wahalifu wenye taaluma mbalimbali, kama vile walimu na mafundi stadi, hupewa fursa ya kuzitumia kwa faida ya jamii bila malipo.
Akizungumzia hali ya sasa ya utekelezaji vifungo vya nje, alisema tangu kuanza kwake katika majaribio la mikoa sita, utekelezaji umeendelea kupanuliwa na kufikia mikoa 18 kati ya 25 ya Tanzania Bara.
Aliitaja mikoa hiyo ni Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Singida, Kagera, Mara, Kilimanjaro, Mwanza, Njombe, Shinyanga, Tanga, Mtwara, Ruvuma, Pwani, Geita, Morogoro, Kagera na Mbeya.
Hata hivyo, alisema katika mikoa hiyo 18 yenye jumla ya wilaya 102, idara ya Huduma kwa jamii inafanya kazi kwenye wilaya 48 pekee ambapo ina uwezo wa kupata wastani wa wahalifu 1,600 kwa mwaka kwenye adhabu mbadala wa kifungo.
Alisema kuanzia 2005 hadi Juni mwaka jana, wahalifu 7,586 waliamriwa na mahakama mbalimbali nchini kutumikia adhabu zao katika jamii chini ya utaratibu wa huduma kwa jamii na probesheni
Alitaja baadhi ya makosa yanayohusika kuwa ni kuruhusu wanafunzi kuolewa, kusababisha ajali barabarani, kusaidia mfungwa kutoroka, shambulio la kawaida, kuua bila kukusudia, kutishia kuua kwa maneno, kupotea kwa mali, kutekeleza familia, kutoa lugha ya matusi na kuingilia amri ya mahakama.
“Chini ya sheria ya probesheni inawahusu wahalifu ambao mahakama inawahukumu muda maalumu wa kuishi kwenye jamii chini ya uangalizi au ufuatiliaji madhubuti kuhakikisha hawatendi kosa lolote hadi muda husika utakapomalizika.
Kuhusu sheria ya Bodi ya Parole inawahusu wahalifu wenye makosa hayo ambapo hutakiwa kutumikia kwanza miaka minne ya kifungo gerezani ndipo kuweza kufikiriwa kuachiliwa kwenda kuishi kwenye jamii bila kutenda makosa yoyote ya jinai kwa muda wote uliobakia wa hukumu za kifungo.

No comments:
Post a Comment