Serikali kupitia Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), itaendelea kutoa mafunzo ya Wafanyabiashara Wadogo na wa Kati (SMEs) ili kuboresha zaidi mahusiano ya kibiashara na wafanyabiashara wakubwa na kampuni.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji), Dk Mary Nagu alisema jijini Dar es Salaam hivi karibu kuwa tayari wajasiriamali 214 wameshafaidika na mafunzo hayo hapa nchini. Miongoni mwa walionufaika, 152 ni wanaume na 62 ni wanawake.
“Kupitia mafunzo haya, wajasiriamali wadogo na wa kati wataunganishwa na makampuni makubwa katika sekta za mawasiliano, ujenzi, kilimo, saruji, madini, viwanda vya samaki, vinywaji baridi na hoteli,” alisema Nagu.
Kwa mujibu wa Dk Nagu, mafunzo hayo yanayojulikana kama ‘Business Linkage’ yana umuhimu mkubwa wa kuboresha mahusiano ya kibiashara kwa wajasiriamali wadogo na wakati na wafanyabiashara wakubwa na kampuni.
“Sisi kama Serikali, tumedhamiria kwa dhati kuisaidia zaidi kada ya wajasiriamali wadogo na wa kati kukua na kuiwezesha kuchangia ipasavyo katika ukuaji wa uchumi wetu wa taifa,” aliongeza.
Waziri Nagu alisema mafunzo hayo yameshafanyika Dar es Salaam, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini (Mbeya), Kanda ya Kaskazini (Kilimanjaro), na Kanda ya Ziwa (Mwanza). Alisema tayari wafanyabiashara 54 walihitimu mafunzo ya usambazaji bidhaa za ndani sawa na asilimia 85.3.
Kwa upande mwingine, Dk Nagu alisema TIC ilishatembelea miradi 99 ya wawekezaji na
kutoa huduma bora na kujenga mahusiano mazuri na wawekezaji hapa nchini.
Alisema Serikali ya Awamu ya Nne, nchini ya Rais Jakaya Kikwete imefanya mageuzi makubwa katika nyanja za uwekezaji hapa nchini na bado inafanya jitihada zaidi katika kuboresha mazingira ya kufanya biashara na kuwekeza.
Kwa mujibu wa taarifa ya hivi karibuni ya Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Biashara na Maendeleo (UNCTAD), mwaka 2013, Tanzania ilikuwa na mitaji toka nje yenye thamani ya Dola za Kimarekani bilioni 12.7 ikiipita Kenya iliyokuwa na Dola za Kimarekani bilioni 3.4 na Uganda Dola za Kimarekani bilioni 8.8.

No comments:
Post a Comment