Wilaya ya Mpanda
mkoani Katavi itafanya operesheni
maalumu ya kuwasaka, kuwakamata na kuwarejesha shuleni
wanafunzi wote waliokatiza
masomo kwa utoro na ambao tayari
wameshazaa.
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Paza Mwamlima
alibainisha hayo wakati wa kikao cha Kamati ya Maendeleo ya Kata
kilichofanyika jana na kubainisha kuwa
atalitumia jeshi la Polisi
kuendesha msako huo unaotarajia kuanza rasmi Julai
mwaka huu.
Pia amewaagiza
wazazi na walezi wa
wanafunzi waliokuwa wakisoma katika Shule ya Sekondari
Mpandandogo, Tarafa ya Kabungu
wilayani hapa ambao
wakatiza masomo yao baada ya kuoa na kuolewa wahakikishe wanawarejesha
shuleni na kuanza masomo mara moja .
“Wazazi na walezi
hakikisheni watoto wenu waliokatiza
masomo kwa utoro, kuolewa au
kuoa pia hata wale
waliokwishazaa mnawarejesha shuleni
kuanza masomo mara moja atakayekaidi
agizo hili atachukuliwa
hatua kali zikiwemo za kisheria...kwani sasa
hatuwezi tena kufumbia macho
jambo hili," alisisitiza.
Mkutano huo wa Kamati ya Maendeleo ya kata
uliofanyika katika Shule ya Sekondari Mpandandogo katika Kata ya Kabungu
ilijumuisha wazazi, walezi na wanafunzi
ili kujadili kwa kina
maendeleo ya elimu ya shule
hiyo ambayo ilishika nafasi ya
mwisho kwa ufaulu wa wanafunzi
katika Mtihani wa Taifa wa kuhitimu
Kidato cha Nne mwaka jana
kwa shule zote za sekondari mkoani Katavi.
Aliongeza kuwa
amelazimika kutoa maagizo hayo kutokana na taarifa kwamba shule ya Sekondari Mpandandogo imekuwa ikifanya vibaya katika
mitihani ya kitaifa kutokana na
sababu mbalimbali zikiwemo utoro uliokithiri.
Sababu zingine
zilitajwa kuwa wanafunzi kukatiza
masomo ambapo wazazi wao wenyewe wanawaoza watoto wao wa kiume
na kuwaozesha mabinti zao
likichukuliwa kuwa ni jambo la
kawaida kabisa.
Awali Mkuu wa
Shule ya Sekondari Mpanda ndogo, Rashid
Msyete alieleza kuwa shule hiyo yenye kidato cha kwanza hadi cha nne
ina idadi ya wanafunzi
165 kati yao wanaume ni 104 na wasichana
61 wakati shule hiyo ina nafasi
ya kusomesha wanafunzi 600 kwa
wakati mmoja.
Naye mzazi
Veronica Godfrey, alieleza kuwa
wanafunzi wengi wa shule hiyo wamekuwa ni watoro kutokana na adhabu kali zinazotolewa na walimu shuleni hapo
pindi mwanafunzi anapokuwa amefanya kosa hata likiwa ni kosa dogo la kinidhamu.
“Hii
adhabu inayotolewa na walimu
wanapowaadhibu wanafunzi maarufu
kama “kunyonya mafuta” ni
kikwazo kikubwa sana kwa wanafunzi
ambapo imesababisha wengi wao
kuwa watoro,” alisema Veronika.
Ndipo Mkuu wa
Wilaya, Mwamlima aliposimama na
kuagiza wanafunzi wa shule hiyo
watoe ufafanuzi wa
adhabu hiyo ndipo alipoelezwa
kuwa adhabu hiyo ya kunyonya mafuta kwamba mwanafunzi anapoadhibiwa
analazimishwa aweke kichwa chake
chini ardhini huku
miguu yake ikiwa
juu hewani.

No comments:
Post a Comment