Sembe nyeusi itakayokuwa ikizalishwa katika kinu kikubwa cha kusaga na kuhifadhi nafaka cha mjini Iringa inatarajiwa kuingia sokoni wakati wowote kuanzia sasa baada ya jaribio la usagaji wake kufanyika juzi kwa mafanikio makubwa.
Kazi ya kusaga sembe hiyo kwa mujibu wa Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), Charles Walwa utafanywa na NRFA baada ya kukabidhiwa jukumu hilo na Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko iliyokabidhiwa kinu hicho na serikali kutoka kwa lililokuwa Shirika la Usagishaji la Taifa (NMC).
Tani tano za mahindi zilitumika katika jaribio hilo lililochukua zaidi ya saa moja mbele ya ushuhuda wa maafisa mbalimbali wa bodi hiyo, wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula na wafanyakazi wa kinu hicho pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dk Christine Ishengoma.
"Kama mlivyoona jaribio limefanikiwa katika mchakato wa kukifanya kinu hiki kianze uzalishaji, hiyo ni baada ya kusimama uzalishaji mwanzoni mwa miaka ya tisini; unga umezalishwa kama mlivyouonaÉhatua inayofuata ni kuchunguza ubora wake," Walwa alisema.
Alisema unga huo utapelekwa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) na Shirika la Viwango Tanzanoa (TBS) ili kuhakiki ubora wake kabla ya uzalishaji wake kuanza rasmi kwa ajili ya kuingizwa sokoni.
Dk Ishengoma alisema kufufuliwa kwa kiwanda hicho kutaongeza
uhakika wa soko la nafaka zinazozalishwa na wakulima wa mkoa ya Iringa na ile ya jirani na hivyo kuongeza wigo wa ajira katika sekta ya kilimo.
Meneja wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini wa NFRA, Abdillah Nyangasa, alisema kinu hicho kimerudi katika hali yake ya kawaida ya uzalishaji baada ya kufanyika kwa matengenezo na ukarabati uliogharimu zaidi ya Sh Milioni 132.
Alisema matengenzo na ukarabati huo ulihusisha pia ununuzi wa mtambo maalumu wa kudhibiti mfumo wa umeme katika kinu hicho. Tayari wamiliki wa kinu hicho wana tani 10,000 zitakazotumika kama mtaji wa awali.

No comments:
Post a Comment