Benki ya TIB imetoa mkopo wa trekta tatu zenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 83, kwa wananchama watatu wa chama cha kuweka akiba na kukopa (Chiringe Saccos) kilichoko mjini Bunda ili waweze kuendesha kilimo vizuri na hatimaye kujiunua kiuchumi.
Mkopo huo umekabidhiwa jana na Afisa Ushirika wa wilaya ya Bunda, Saulo Lunyeka, kwenye hafla fupi iliyofanyika katika ofisi za chama hicho mjini Bunda.
Akikabidhi mkopo huo Lunyeka alisema kuwa, umetolewa na benki hiyo ili wakulima hao ambao ni wanachama wa Saccos waweze kufanya kazi yao ya kilimo kwa ufanisi zaidi, badala ya kulima kwa kutumia majembe ya mikono.
Aliwaasa wanachama hao kurejesha mkopo huo kwa muda muafaka, ili wanachama wengine nao waweze kukopeshwa na kuongeza kuwa wananchi wanapaswa wajiunge kwenye vikundi na vyama vya kuweka akiba na kukopa ili waweze kupata fursa ya kukopesheka na vyombo vya kifedha.
"Mimi nipende tu kuwaasa ndugu wanachama kwamba zingatieni
msharti ya mkopo huu, rejesheni kwa wakati muafaka ili wnzenu pia waweze kukopesheka, lakini pia nitumie fursa hii kuwaambia wananchi wengne wajiunge kwenye vikundi na Saccos kama hii ili waweze kupata fursa ya kukopesheka kwenye vyombo vya kifedha," alisema.
Mwenyekiti wa Saccos hiyo, Robert Masatu, alisema walianza
mchakato wa kuomba mkopo huo mwaka 2012 na kwamba trekta hizo zitawasaidia wakulima kulima maeneo makubwa ya mashamba na kwa wakati muafaka kulingana na msimu wa mvua ulivyo.
Masatu alisema kuwa matarajio yao ni kuhakikisha wanachama wote wa Chiringe Saccos ambao ni 69, wanapata mkopo huo wa trekta kwani wengi wao ni wakulima, ili waweze kulima kwa kutumia teknorojia hiyo badala ya kutumia majembe ya mikono, ambayo hutumia muda mwingi kulima na kuwachosha kwa
haraka.
Wakulima waliopata trekta hizo ni Robert Masatu, Opigi Ocharo na Nyerere Odera, ambao wote ni wakazi wa wilayani Bunda, na kwamba watarejesha mkopo huo kwa muda wa miaka minne, ambapo kila miezi mitatu watakuwa wanarejesha kiasi cha Sh milioni 3.9.

No comments:
Post a Comment