Idadi ya wagonjwa wa dengue mkoani Dar es Salaam
inazidi kupungua kila siku.
Ofisa Ufuatiliaji wa Magonjwa wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alex Mkamba alisema jana kuwa hospitali za Dar es Salaam zilipokea wagonjwa saba.
Alisema kupungua kwa wagonjwa, kunaashiria kuwa ugonjwa huo unakaribia kumalizika.
“Hali sasa ni nzuri, tunavyozidi kwenda hali inapungua leo tumepokea wagonjwa saba tu, jambo ambalo linatia moyo,” alisema Mkamba.
Alisema katika wagonjwa hao saba, Hospitali ya Temeke ilipokea wagonjwa wawili, Hospitali ya Mwananyamala wagonjwa watano na Hospitali ya Amana haikupokea wagonjwa.
Mkamba alisema ili kutokomeza ugonjwa huo, serikali inaendelea kufanya ukaguzi ili kuhakikisha maeneo yote yenye vichaka au mazingira machafu, yanayosababisha mbu kuzaliana, yanasafishwa. Hadi sasa Mkoa wa Dar es Salaam umekwishafanya ukaguzi katika kaya 2,500.

No comments:
Post a Comment