Rais
Jakaya Kikwete amemteua Andrew Nyumayo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la
Mzinga lililopo mkoani Morogoro.
Kwa
mujibu wa taarifa ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa,
Job Masima, uteuzi huo umeanza Mei 6, mwaka huu.
Nyumayo
amewahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini kabla ya kustaafu, ikiwa ni
pamoja na kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.
Sambamba
na uteuzi huo wa Mwenyekiti, pia Bodi hiyo itakuwa na wajumbe wafuatao: Luteni
Jenerali Samweli Ndomba ambaye ni Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi ambaye
katika Bodi hiyo atakuwa Makamu Mwenyekiti, Luteni Jenerali (mstaafu) Martin Mwakalindile na
Meja Jenerali Dk Charles Muzanila, ambaye ni Meneja Mkuu wa Shirika la Mzinga.
Wajumbe
wengine ni Meja Jenerali (mstaafu) Said Omar, Meja Jenerali (mstaafu) Festo
Ulomi, Kanali Dk Wema Wekwe, John William Nyoka na Adalus Magere.
No comments:
Post a Comment