![]() |
| Mmoja wa walimu akiwajibika darasani. |
Hata hivyo, Katibu Mkuu wa Idara ya Utumisi wa Walimu (TSD), Subira Mwakibete alisema utaratibu wa kuhuisha taarifa za walimu ni wa kawaida na kusisitiza hakuna majalada yaliyopotea.
Alisema ofisi yake iliyo chini ya Tume ya Utumishi wa Umma, inafanya zoezi la kuhuisha taarifa za walimu kwa lengo la kuboresha orodha ya walimu kulingana na madaraja yao.
"Kazi yetu ni kutunza 'seniority list' ya walimu wote kwenye halmashauri, ambayo inaonesha wameanza lini kazi na mara ya mwisho ni lini walipanda cheo na kama wapo wanaopaswa kupanda", na kuongeza
"taarifa hizi zitasaidia kujua ni walimu wapi wanaotaka au wanakaribia kustaafu, kama wamethibitishwa kazini na kuonesha taarifa zaidi kama wamejiendeleza", alisema Mwakibete.
Mwandishi alipata taarifa za kuwepo upotevu wa majalada ya walimu kutokana na ofisi hiyo kuhama kutoka jengo la Anautoglou kwenda Ubungo Plaza kabla ya kurejea eneo hilo.
Hata hivyo, Mwakibete alisisitiza kuwa utaratibu huo, umekuwa ukifanywa kwenye wilaya nyingine.
Alisema inavyoonekana walimu wasio na vyeti, ndio wenye wasiwasi wa kupeleka taarifa zao na kuongeza kama wamepoteza vyeti, au nyaraka nyingine zinazohitajika, upo utaratibu wa kutoa taarifa za upotevu.
Aidha, Mwakibete alisema hadi Aprili mosi mwaka huu ni walimu 97 tu ndio walioitikia mwito huo, kati ya walimu 105 kwa kupeleka taarifa zao katika Manispaa ya Ilala na kuwataka ambao hawajapeleka kufanya hivyo ndani ya wiki moja.
Shule ambazo walimu hawajapeleka taarifa zao, wakuu wao wameomba muda wa zaidi ili wakamilishe, kwa kuwa yapo matatizo mbalimbali yakiwemo ya walimu kuwa masomoni.
Baada ya zoezi hilo kukamilika kwenye shule za msingi, litahamia kwenye shule za sekondari.

No comments:
Post a Comment