Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete atakuwa mgeni rasmi katika Kongamano la Wanafunzi wa Vyuo Vikuu vilivyopo Dodoma, litakalojadili mustakabali wa mtoto wa kike katika mazingira ya sasa.
Hayo yalisemwa na mjumbe wa wanafunzi hao Jasmine Awadh kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Jasmine alisema kupitia kongamano hilo, wanafunzi wa kike wa vyuo vikuu vya Dodoma watapata fursa ya kujadili masuala yanayomhusu mtoto wa kike katika kujitambua na kujua namna ya kukabiliana na mazingira ya sasa.
Alisema kaulimbiu ya Kongamano hilo ni ‘Wanawake tukithubutu tunaweza’ na kwamba mada nne za kuwahamasisha wanawake katika uongozi, afya ya uzazi, nafasi ya mtoto wa kike katika Katiba mpya, na mada kuhusu malengo na kujitambua, zitawasilishwa.

No comments:
Post a Comment