Sunday, April 13, 2014

NIDA YAHIMIZA WAPEMBA KUJITOKEA KWA WINGI

Mamlaka ya vitambulisho nchini (Nida) imewataka wananchi wa Pemba kujitokeza kwa wingi katika uandikishaji wa vitambulisho vya taifa kwa kuwasilisha vielelezo vyote muhimu ikiwemo vyeti vya kuzaliwa.
Ofisa uhusiano wa Nida, Thomas William aliwataka wananchi kuwasilisha vielelezo muhimu ambavyo vitasaidia kukamilisha uandikishaji huo.
Alivitaja vitu muhimu vinavyohitajika kupatikana katika uandikishaji huo kuwa ni cheti za kuzaliwa, cheti cha kumaliza shule pamoja na kitambulisho cha Mzanzibari mkaazi.
Aidha aliwataka masheha wa kisiwa cha Pemba kutoa ushirikiano na kusisitiza, "Tunawaomba masheha kutusaidia katika uandikishaji wa vitambulisho vya taifa kwa ajili ya kurahisisha na kukamilisha haraka".
Katika uandikishaji huo watumishi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na taasisi za Muungano wataanza kusajiliwa.

No comments: