Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Fabian Massawe amesema kuwa baadhi ya sheria mama, mila, desturi na baadhi ya dini nchini ni moja ya changamoto zinazodidimiza maendeleo ya watoto wa kike.
Amesema changamoto hizo, zinafanya watoto wa kike, kushindwa kuendelea na masomo huku wakiolewa katika umri mdogo.
Massawe alisema hayo juzi ofisini kwake wakati akizungumza na mwandishi, ambapo pia alieleza changamoto mbalimbali, zinazorudisha nyuma maendeleo ya watoto hao.
Alisema Serikali na wadau mbalimbali, wamejitahidi kupambana na changamoto zinazowakumba watoto wa kike, ikiwemo kuozeshwa katika umri mdogo.
Lakini, alisema changamoto hizo bado ni vikwazo vikubwa kwa watoto wa kike.
Alisema kikwazo kingine ni Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971, ambayo inasema mtoto wa kike akifikisha miaka 14 ni mtu mzima anao uwezo wa kuolewa.
Alisema pia kuwa mila, desturi na baadhi ya dini zinaruhusu wanaume kuoa wanawake wengi na kwamba mtoto akishavunja ungo au kubalehe, huyo ni mtu mzima, anaweza kuolewa au kuoa.
“Sheria hii ya Ndoa inahitaji mabadiliko makubwa, kwani imekuwa kikwazo kikubwa pale tunapopambana na tatizo la kuwakomboa watoto wa kike. Lazima tulipiganie hili liingie kwenye Katiba mpya ili sheria hiyo itamke kuwa kumuozesha mtoto mdogo ni kumuonea na kumnyima haki yake. Tunataka pia baadhi ya makabila na baadhi ya dini zetu, zinazoruhusu kuozesha watoto baada ya kubalehe au kuvunja ungo na kuoza wanawake wengi ambao wengi wao ni watoto, wawajibishwe, kwani ni kuwanyima haki watoto” alisema Massawe kwa uchungu.
Alisema asilimia 51 ya Watanzania ni wanawake. Alisema wanawake wanatakiwa kuelimishwa kwa nguvu zote, kwa sababu wakipata elimu wana uwezo wa kuleta maendeleo ya haraka.
Alisema mtu anapomuelimisha mtoto wa kike, huwa ameelimisha jamii, kwa sababu wanawake ndio wanaohudumia zaidi jamii na wanapopata mitaji, huitumia vizuri katika kukuza maendeleo yao na ya jamii.

No comments:
Post a Comment