Kwa mara ya kwanza matumaini ya kupatikana kwa mabaki ya ndege ya Malaysia yameanza kuwa na nguvu baada ya meli ya China kupokea tena ishara inayodhaniwa imetoka katika kisanduku cheusi.
Kauli hiyo imetolewa na Australia ambayo inaratibu utafutaji wa ndege hiyo ya Malaysia iliyokuwa na mruko namba MH370.
Mkuu wa Jeshi la Anga la Australia, Angus Houston, anayesimamia operesheni hiyo alisema kwa meli ya China kwa mara ya pili imepokea ishara ya kielektroniki baada ya ile ya kwanza iliyopatikana Ijumaa.
Houston, amesema mwito huo wa kielektroniki unatoa matumaini.
"Hii ni hatua muhimu na inayotia matumaini, lakini ninachotaka kutilia mkazo kwenu ni kuandika habari hii kwa umakini,” Houston aliwaambia waandishi wa habari akihadharisha kuwa bado mapema kusema waziwazi kwamba hakuna shaka hiyo ni ishara ya kupatikana kwa kisanduku hicho ambacho kwa kawaida hurekodi mwenendo wa ndege.
"Nimeweka bayana, kuwa viashiria hivi na vitu vyeupe vilivyobainika kuelea katika aneo hilo bado havijathibitishwa kama vina uhusiano na ndege iliyopotea,” alisema.
"Jana (juzi) alasiri kwa mara ya pili kumekuwapo na ishara za elektroniki kiasi cha kilomita mbili kutokana wito wa kwanza uliposikika. Ishara ya pili imedumu kwa sekunde 90,” alisema.
Kasi ya utafutaji wa ndege hiyo, ambayo ilitoweka wakati ikisafiri kati ya Kuala Lumpur na Beijing Machi 8, mwaka huu, umeongezeka kwa kadri muda unavyosonga ili kuwahi muda ambao kwa kawaida betri ya kisanduku hicho inakuwa hai.
Wataalamu wanasema betri hiyo huisha nguvu baada ya siku 30. Ndege hiyo ya Boeing 777 ilipotea ikiwa na watu 239, huku watu zaidi ya 150 ni raia wa China.

No comments:
Post a Comment