![]() |
KUSHOTO: Mr Nice alipojeruhiwa kwa chupa baada ya kutuhumiwa kutembea na mke wa mtu. KATIKATI: Mr Nice enzi zake alipokuwa 'ananuka pesa'. KULIA: Mr Nice alivyo sasa. |
Katika hali isiiyokuwa ya kawaida msanii Lucas Mkenda maarufu kwa jina la Mr Nice ameibuka na kueleza sababu zilizomfanya kufilisika licha ya kuwahi kuwa na zaidi ya Shilingi bilioni moja na nusu kwenye akaunti zake tofauti.
Akiongea na Xdeejayz Tanzania msanii huyo ambaye kwa sasa yupo nchini kwa muda mfupi kabla ya kurudi tena nchini Kenya alikohamishia makazi na kufanyia shughuli zake za kimuziki huko.
Akizungumza na mwandishi wetu kwenye ukumbi wa mpya wa burudani wa Full Stop uliopo Mwanamboka Kwa Manyanya Kinondoni Jijini Dar ambapo alisema kuwa dunia imemfanyia kitu kibaya na hafahamu nini kimetoka katika maisha yake.
Mr Nice alisema kuwa anashindwa kuelewa kwa nini maisha yamempiga kiasi hicho kwani pesa yote aliyokuwa anaipata alikuwa anaipata kwa jasho lake. "Kaka naweza kusema hii ni mipango ya Mungu tu kwani sikuwahi kumdhurumu mtu wala kuiba cha mtu pesa yote nilikuwa naipata kwa hali naweza kusema hii ni mipango ya Mungu tu wala si mkono wa mtu," alisema mwanamuziki huyo kwa huzuni.
Aidha mwanamuziki huyo anasema, "Niliwahi kuwa na zaidi ya Shilingi bilioni moja na mia tano kwenye benki tofauti hapa nchini, pesa hizo zilitokana na kufanya shoo nyingi za nje ya nchi kama Marekani, Uingereza, Ujerumani, Sweden, Uholanzi, Dubai, Afrika Kusini na kwingineko na kila shoo nilikuwa napata pesa 'ndefu' sana," alisema.
Hata hivyo, Mr Nice anasema kuwa hizo ni nchi za mbali lakini bado shoo za alizokuwa anazifanya nchi za Kongo, Zambia, Uganda, Rwanda, Kenya.
Moja ya shoo ambayo akiikumbuka huwa inamtoa machozi ni ile ya nchini Rwanda ambayo siku anashuka Uwanja wa Ndege alikuta kitu cha kushangaza sana.
Anasema alikuta umati mkubwa wa watu ukimsubiri akiwamo Waziri wa Michezo wa nchi hiyo pamoja maofisa wa juu wa Polisi na Jeshi huku kukiwa na zulia jekundu kisha akapigiwa saluti huku akisindikizwa na mizinga ishirini na moja.
Hata hivyo msanii huyo anasema alifikia uamuzi wa kujiita 'The Millionaire Mr Nice' baada ya kuingia mkataba na kampuni ya bia nchini (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager ambapo alifanya shoo mikoa yote ishirini na tano ya Tanzania kwa nyingi na kufanya kuwa msanii mwenye pesa nyingi kuliko yeyote Afrika Mashariki.
Jeuri ya fedha aliyokuwa nayo msanii huyo enzi zake ni msafara wake uliosheheni wapambe ambao ulikuwa na msululu wa magari zaidi ya manane kwenye mizunguko yake huku yakiwa hayazimwi viyoyozi masaa ishirini na nne hata kama hayana watu ndani.
Aidha Mr Nice alimaliza kusema kuwa anawashauri wasanii wa sasa kujifunza kwa waliopita ili nao yasije kuwakuta kama yaliyowakuta wao.

No comments:
Post a Comment