Katika kutafuta mwarobaini wa ajali za barabarani, polisi imeanza kutumia kamera maalumu za kudhibiti mwendo kasi, zenye uwezo wa kupiga picha za mnato na video.
Pia, kamera hizo zina uwezo wa kuonesha namba ya gari na muda, ambao taarifa husika zimechukuliwa.
Kamera hizo ambazo zinaweza kufanya kazi bila kuwepo askari, zitawekewa mwendo unaotakiwa, ambao gari litakalozidisha, kamera zitarekodi na baadaye kufanyiwa uchambuzi na magari husika kukamatwa.
Taarifa hiyo sanjari na inayohusu askari 10 wa usalama barabarani, waliofukuzwa katika kipindi cha miezi mitatu sasa kwa kukiuka sheria na maadili ya kazi zao, ikiwemo kujihusisha na vitendo vya rushwa, ilitolewa jana na Kamanda wa Polisi, Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga.
Alikuwa akitoa taarifa kuhusu vyanzo vya ajali zilizotokea mwaka jana.
Alisema kamera hizo, zitawezesha kuchukua picha na mwendokasi wa gari, likiwa umbali wa meta kati ya 100 na 500. Aidha wanaweka utaratibu wa kulinda kamera zising’olewe.
"Baada ya kuchukua picha hizo, tuna uwezo wa kuziweka kwenye kompyuta na kufanya uchambuzi kisha magari yatakayokuwa yamebainika, yatachukuliwa hatua,” alisema.
Alisema kamera hizo ni za kisasa zaidi, tofauti na zilizokuwa zikitumika awali, ambazo ilikuwa lazima awepo askari wa kusoma mwendo kasi.
Pia, hazikuwa na uwezo wa kutoa namba za gari wala picha.
Alisema kwa kamera za sasa, zitaondoa malalamiko yaliyokuwa yakijitokeza miongoni mwa madereva, wakidai wamebambikiwa kesi.
Mpinga alisema kwa sasa kamera hizo zipo tatu tu, ambazo wataziweka katika maeneo hatarishi, yaliyokithiri kwa ajali. Miongoni mwake ni Mlandizi hadi Chalinze.
Hata hivyo, alisema mkakati uliopo ni kuhakikisha zinapatikana kamera nyingi zaidi.
Mpinga alisema kwa kushirikiana na Wizara ya Ujenzi, wako katika mchakato wa kutengeneza mfumo, utakaofanya uchambuzi sahihi kitaalamu katika kutambua maeneo hatarishi.
Mfumo huo, unatengenezwa na kampuni kutoka Australia.
Akizungumzia kufukuzwa kazi kwa askari hao 10 wa kikosi cha Usalama Barabarani, Mpinga alisema sita wanatoka Mkoa wa Pwani na waliobaki ni kutoka Mkoa wa Kipolisi wa Temeke.
“Askari hawa wamefukuzwa kazi baada ya kushitakiwa kijeshi katika mikoa yote na kupatikana hatia ikiwemo kudhalilisha jeshi na kufanya lisiaminike kwenye jamii,” alisema.
Akitoa takwimu za ajali alisema kwa mwaka jana, makosa ya kibinadamu yalichangia ajali kwa asilimia 75, kutokana na uzembe wa madereva, mwendo kasi, kupita magari mengine bila hadhari, uzembe kwa wapanda pikipiki na ulevi.
Mpinga alisema pia ongezeko la vijana wanaojihusisha na biashara ya kubeba abiria kwa pikipiki wasio na sifa wala weledi, ni sababu nyingine ya ongezeko la ajali.
Kwa mujibu wake, Desemba, 2009 pikipiki zilizokuwa zimesajiliwa na Mamlaka ya Mapato (TRA) zilikuwa 207,465.
Desemba mwaka jana, pikipiki zilizosajiliwa ni 697,259 kukiwa na ongezeko la pikipiki 489,794.
Mpinga alisema hali ya barabarani na mazingira yake, ilichangia ajali kwa asilimia nane huku ubovu wa magari ukichangia kwa asilimia saba.
Alisema katika robo ya kwanza ya mwaka huu, kulikuwa na makosa 240,350 ikilinganishwa na robo ya kwanza ya mwaka jana, ambayo makosa ni 153,333 kukiwa na ongezeko la makosa 87,017.
Mpinga alisema kutokana na takwimu hizo, wamekuwa na mikakati mbalimbali ya kupunguza ajali hizo kama kutumia kamera hizo mpya, kuimarisha ukaguzi wa ratiba za mabasi na kuongeza matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama).
Alisema kupitia Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN), watapunguza vizuizi vya polisi kwa magari ya aina zote, kutoka 15 vya sasa katika barabara ya Dar es Salaam hadi Rusumo hadi kubakia vitatu ambavyo ni Vigwaza, Manyoni, Nyakanazi.
Aidha, wakati mchakato huo ukiendelea, vizuizi vya polisi kutoka Dar hadi Rusumo vitakuwa sita, Dar es Salaam hadi Tunduma/Kasumulo vitabaki sita na Dar es Salaam hadi Namanga hadi Holili vitakuwa vitatu.
Alisema mchakato wa matumizi ya leseni mpya, kudhibiti mienendo ya madereva wa kuweka nukta nundu kwenye leseni upo katika hatua za mwisho na umesharidhiwa na Wizara ya Sheria na Katiba.
Kwa mujibu wa takwimu, kumekuwa na ongezeko la matukio 264 ya ajali za barabarani kwa mwaka jana ambao ni sawa na asilimia 1.1, ikilinganishwa na mwaka juzi ambao matukio yalikuwa 23,578.
Mpinga alitaja maeneo yaliyoongoza kwa ajali ni Kinondoni, Ilala, Temeke (Dar es Salaam), Kilimanjaro na Pwani.
Ajali 3,427 zilisababisha vifo mwaka jana, sawa na ongezeko la asilimia 3.0, ikilinganishwa na mwaka 2012 ambapo kulikuwa na vifo 3,328.
Alisema ajali zilizosababisha majeruhi kwa kipindi hicho ni 11,307, sawa na ongezeko la asilimia 2.6, ikilinganishwa na mwaka 2012 ambapo kulikuwa na majeruhi 11,021.

No comments:
Post a Comment