Arsenal inakabiliwa na matatizo ya wachezaji wake watatu kuwa katika hatihati ya kuikabili Wigan Athletic katika nusu fainali ya Kombe la FA kesho, huku Aaron Ramsey akitarajiwa kuanza.
Mkakati wa kikosi cha Arsene Wenger wa kusaka taji la kwanza tangu 2005 unaendelea kesho kwa kukabiliana na mabingwa watetezi, na wanaingia katika pambano hilo wakiwa hawajashinda mechi nne mfululizo katika Ligi Kuu na hivyo kutibua mbio za kuwania nafasi ya kufuzu Ligi ya mabingwa Ulaya.
Na nafasi ya Arsenal kuelekea kumaliza ukame wa mataji unaonekana kuwa hatarini kutokana na matatizo ya majeruhi, kwani viungo watatu Tomas Rosicky na Alex Oxlade-Chamberlain wako shakani kucheza, wakati mlinzi wa kushoto Kieran Gibbs naye yuko shakani kutokana na kuumia kifundo cha mguu.
Lakini licha ya hatari hiyo, Ramsey aliyeingia katika kipindi cha pili walipochapwa na Everton mwishoni mwa wiki, huenda akaanza kwa mara ya kwanza tangu Desemba 26, mwaka jana.
“Aaron Ramsey yuko tayari kuanza dhidi ya Wigan,” alisema Wenger.
“Lakini kuna mambo mengi hayako vizuri. Gibbs, Rosicky na Oxlade-Chamberlain wote wako shakani.”
Wenger pia alieleza kuhusu hali ya mlinzi wa kati, Laurent Koscielny na kiungo mchezeshaji Mesut Ozil, ambao wamekuwa nje kwa majeraha ya kano na nyonga.
“Ozil anaweza kurejea Jumamosi ijayo (dhidi ya Hull City),” alisema. Koscielny anaweza kurejea Jumanne (dhidi ya West Ham).”

No comments:
Post a Comment