![]() |
| Semina ya Bunge Maalumu la Katiba. |
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba mapema leo asubuhi wamepitisha kwa kauli moja Kanuni zitakazoongoza vikao vya bunge hilo.
Mara baada ya kupitishwa, Mwenyekiti wa Muda, Pandu Ameir Kificho, alitangaza rasmi kufunguliwa milango kwa wajumbe wanaoona wana sifa za kuwania nafasi za Mwenyekiti na Makamu wake kuanza kuchukua fomu hizo za kugombea nafasi hizo.
Mbali na hilo, Kificho alitangaza kuwa uchaguzi utafanyika kesho saa 10 jioni ili kuweza kujaza nafasi hizo tayari kwa kuanza rasmi vikao vya kuichambua Rasimu ya Katiba.
Kupitishwa huko kwa Kanuni kumekuja baada ya mvutano mkali uliodumu kwa takribani wiki tatu ulioambatana na matusi miongoni mwa wajumbe katika kujadili Rasimu ya Kanuni hizo.
Licha ya kupitishwa kwa Kanuni hizo, wajumbe hao wameshindwa kufikia makubaliano ya kura gani, itumike wakati wa kupitisha uamuzi wa ibara za rasimu ya Katiba mpya.
Kura inayobishaniwa na wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, ni kama iwe ya siri au wazi, jambo lililogawa Bunge hilo katika makundi mawili, yanayotofautiana kuhusu namna gani uamuzi ufanyike ndani ya Bunge hilo.
Kutokana na jambo hilo kushindwa kupata muafaka, kuhusu aina ya upigaji kura kwenye kufanya uamuzi, sasa Bunge hilo limeamua kupitisha rasimu ya Kanuni huku kifungu hicho cha kufanya uamuzi, kikieleza tu kuwa uamuzi utafanywa kwa kupiga kura.
Mwenyekiti wa Muda wa Bunge Maalumu, Pandu Ameir Kificho, alitangaza hatua hiyo jana, baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya Kanuni, Profesa Costa Mahalu, kuliambia Bunge hilo kuwa kifungu hicho, sasa kitasomeka tu kwamba uamuzi wake, utafanywa kwa kupiga kura.
Kificho ambaye aliingia ukumbini saa 6.15 mchana badala ya saa tano aliyoahidi siku ya Jumamosi, aliomba radhi kuchelewa kwa vile alikuwa anaendelea kushauriana na Kamati ya Kumshauri kuhusu kanuni, ambayo ilikuwa inaendelea kufanya marekebisho ya kanuni hasa kwa Kanuni ya 37 na 38.
Profesa Mahalu aliliambia Bunge hilo, kuwa wamekamilisha kazi katika kanuni hizo za 37 na 38, ambazo zinaeleza namna ya kufanya uamuzi utakuwa ni kupiga siri ambayo itaamriwa na Bunge hilo. Kamati hiyo ambayo awali ilipendekeza kura iwe ya siri, sasa imesema tu kuwa mambo yote yataamriwa kwa kura.
Kwa hatua hiyo ya Kamati ya Kanuni, ni wazi kuwa uamuzi wa namna gani litafikia maamuzi umewekwa kiporo.
Kificho katika maamuzi yake, alisema kuwa Bunge lingepitisha kanuni, ambazo zimesharidhiwa kwenye semina hiyo na hizo mbili bado zitatafutiwa ufumbuzi na Kamati ya Maridhiano.
Tangazo hilo la Kificho lilizua mjadala mkubwa, hali iliyoonesha baadhi ya wajumbe kutokubaliana na hatua hiyo, ambao baadhi yao walitaka Bunge hilo lipige kura ya kumaliza suala hilo na sio kuendelea kuliweka kiporo, kama alivyotaka Mwenyekiti wa Muda. Wengine wakapendekeza Bunge livunjwe.
Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila alisema kwa kuwa wabunge wanaendelea kutafuna posho, ambayo ni kodi ya wananchi, lakini wameshindwa kupata muafaka wa jambo hilo, ni vyema Bunge hilo livunjwe na waletwe watu wengine, wenye dhamira safi ya kufanya kazi hiyo.
“Tangu tuanze hapa tunavutana juu ya jambo hili na kanuni hapa zimekwama na hakuna uamuzi mbadala, kama jioni tukija hapa jambo hili bado halijapata muafaka, ni vyema Bunge hili livunjwe maana hatuwezi kuendelea kupata posho wakati kazi hazifanyiki,” alisema Kafulila.
Kificho alimjibu mbunge huyo kuwa Bunge hilo, limeanza kwa tangazo la Rais ;na Rais ndiye mwenye mamlaka ya kulivunja ;na sio vinginevyo.
Hezekiah Oluoch alisema kwa kuwa Kamati ya Maridhiano, imekutana kwa siku tatu na imeshindwa kupata ufumbuzi ni bora suala hilo lipigiwe kura.
“Naomba Sekretarieti itugawie karatasi tuamue jambo hili, wewe tulikuchagua kwa siri na suala hili tutalipiga kwa siri,” alisema.
Hoja ya Oluoch ilikuwa kuwa Bunge haliwezi kuendelea na kazi yake ya kuridhia kanuni nusu, wakati vifungu vingine havijafikia na kumtaka Mwenyekiti atendee haki Bunge hilo ili vifungu hivyo viwili, vipitishwe na wabunge wenyewe.
Diana Chilolo ambaye ni Mbunge wa CCM Viti Maalumu, alisema kama ni kura inapigwa kuhusu vifungu hivyo, ipigwe kura ya wazi.
“Kwa nini tunapata kigugumizi juu ya jambo hili? Kama Kamati ya Mashauriano imekwama kupata muafaka tupige kura na wananchi wanataka kura iwe ya wazi.”
Mbunge huyo ambaye wakati anatoa hoja hiyo, alikuwa akizomewa alisema; “ Kuzomea sio jambo la busara na ni tabia mbaya na Mungu hataki, hivyo mimi nashauri tupige kura ya wazi kuhusu vifungu hivyo”.
William Lukuvi ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, alisema kwa kuwa vimebaki vifungu viwili ni vyema Bunge hilo, liendelee na ratiba yake na hizo kanuni kiporo zitapitishwa baadaye baada ya Kuunda Kamati ya Kanuni za Bunge.
Hoja hiyo ya Lukuvi, pia ilisababisha azomewe, lakini akawa ngangari na kuendelea kusema “Nyie zomeeni… lakini mimi ni sugu wa kuzomewa, hapa ninachokisema ni kwamba kama mnataka semina hii tumalize kila jambo basi hakuna hata haja ya kuunda Kamati ya Kanuni ya Kudumu.
“Tusijidanganye kuwa hizi kanuni zitakuwa kamili kwa uhai wote wa Bunge hili, kuna mambo yanaweza kuletwa hapa kwa ajili ya marekebisho na ndio maana kunaundwa Kamati ya Kanuni; hivyo suala hili baadaye litaletwa na kamati hii ni vyema kwa sasa tuendelee na mambo mengine,” alisema Lukuvi.
Lukuvi alisema sio jambo jema kupiga kura kuamua jambo hilo kwani litagawa Bunge hilo. “Hata tukipiga kura hapa kuna kundi litashinda na lingine litashindwa, iweje tuwe na Bunge ambalo limegawanyika kwenye mambo ya Katiba?
Mjumbe wa Kamati ya Kanuni, George Simbachawene, alimkosoa Lukuvi na Kificho kuwa vifungu hivyo, haviwekwi pembeni, bali kanuni zitakazopitishwa zitahusisha vifungu hivyo viwili, kwani vinatamka kuwa uamuzi utafanyika kwa kura, ila haielezi aina ya kura itakayopigwa.
“Vifungu hivi havitaji siri au wazi, ila vinasema tutaamua kwa kura, tumefikia hapo maana wananchi wanalalamika tunakula posho bila kazi, ni vyema tuanze kazi kwa kuapisha watu na kuchagua Mwenyekiti na twende kwenye kamati.
“Tutakapofikia wakati wa kutoa uamuzi kila mtu atakuwa ameshajiuliza na Kamati ya Kanuni italeta jambo hilo na sisi kama Bunge tutaamua ni aina gani ya kura ipigwe na wakati huo, Kamati ya Maridhiano naamini itakuwa imefikia hatua nzuri,” alisema Simbachawene.
Baada ya maoni hayo ya Simbachawene, wajumbe wengi walisimama kutaka kutoa maoni, lakini Kificho alisema kuwa kilichofikiwa kwenye Kamati ya Kanuni, ndicho mbacho kimeamriwa kwenye Kamati ya Mashauriano hivyo ni vyema jioni wapitishe kanuni hizo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Felix Mkosamali, ambaye ni Mbunge wa Muhambwe alikosa uvumilivu baada ya kuitwa mtoto na kusababisha majibizano ya ‘matusi’ miongoni mwa wajumbe.
Majira ya saa 10 jioni baada ya Mwenyekiti wa Muda, Pandu Ameir Kificho kufungua Bunge, Mkosamali alisimama kuomba muongozo, lakini aliambiwa asubiri na atapewa nafasi wajumbe wa Bunge hilo wakifika nusu yake.
Hata hivyo, baada ya dakika kadhaa, James Mbatia ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha NCCR Mageuzi, chama anachotoka Mkosamali, alisimama na kuomba muongozo.
Alipokubaliwa alisema kutokana na kutopata nakala ya Rasimu ya Kanuni, hawataweza kujadili rasimu hiyo na Kificho, akamuambia ndiyo maana amesimamisha Bunge kwa muda ili nakala wapewe wajumbe.
Kutokana na hatua hiyo, Mkosamali alisimama na kusema; “Mwenyekiti samahani nakuheshimu sana lakini mimi umeninyima nafasi ya kuzungumza lakini mjumbe (Mbatia), umempa nafasi hivi sivyo njia sahihi ya kuendesha Bunge.”
Baada ya kumaliza, ikasikika sauti ya mbunge mwanamke, ikamjibu “mtoto mdogo hana adabu” na alipomaliza ikatokea sauti nyingine ya Mbunge mwanamume, akajibu “Kubwa jinga halina adabu.”
Naye Mkosamali akajibu; “hakuna mtoto mdogo aliyeishinda CCM.”
Kutokana na malumbano hayo, yaliyodumu kwa dakika tano, Kificho akasema; “hakuna mtoto hapa watu wote ni wajumbe”.
Alipomaliza kutoa kauli hiyo, Kificho akaahirisha Bunge saa 10:27 jioni hadi saa 12:00 jioni, kutokana na kazi ya kudurufu kanuni kutomalizika na kupewa wajumbe ili waendelee kuziridhia.

No comments:
Post a Comment