![]() |
| Ujenzi wa Barabara ya Mabasi ya haraka. |
Badala yake manispaa hiyo imemtaka Wakala wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka Dar es Salaam (DART) kuwaondoa wafanyabiashara hao ndipo iendelee na ujenzi huo kwa kuwa tatizo liko kwenye eneo la mradi wao.
Mwanzoni mwa wiki Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadiki aliiagiza Manispaa ya Kinondoni kuwaondoa haraka wafanyabiashara hao ili kumpisha mkandasi anayejenga barabara hiyo Kampuni ya Strabag aweze kufanya kazi yake baada ya kutoa malalamiko yake kuhusu kero ya machinga hao.
Ofisa Habari wa manispaa hiyo Sebastian Mhowera alisema jana kwamba wao hawahusiki na kuwaondoa wafanyabiashara hao na kwamba suala hilo litabaki kuwa kwa watu wa DART.

No comments:
Post a Comment