Sunday, March 2, 2014

CHEKA KIMYA-KIMYA...

Bosi mmoja alikuwa na desturi ya kunywa mvinyo kabla ya kulala na kuhifadhi chupa chini ya kitanda. Baada ya kugundua mvinyo wake unazidi kupungua kwa kasi, bosi akahisi kuna mtu anayemwibia na hivyo akaweka mtego.
Siku ya siku akamnasa kijana wake wa ndani akimimina mvinyo. Basi bosi kwa kutaka kumdhalilisha yule kijana akapanga amfanye akiri mbele ya mke wake wakati kijana akiwa jikoni. Bosi: "Jeromeee". Kijana: "Naam bosi!" Bosi: "Nani anaiba mvinyo wangu?" Kijana akanyamaza. Baada ya kuuliza mara kadhaa bila majibu bosi akainuka kwa hasira na kwenda jikoni huku akifoka, "Kwanini hujibu?" Kijana: "Nashangaa, huku jikoni ukiita nasikia ila swali halisikiki! Kama unabisha hebu kaa huku jikoni halafu mie niende sebuleni nikuite!" Bosi akaakaa jikoni na kijana akaenda sebuleni. Kijana: "Bosiiiiiii!" Bosi: "Naam!" Kijana: "Usiku huwa unaenda kufanya nini chumbani kwa hausigeli?" Bosi akabaki kimyaa. Ghafla akatoka jikoni na kwenda kwa mkewe huku akijitetea, "Mke wangu nimeamini ukikaa kule husikii swali lolote..."

No comments: