Moja ya aina ya mashine za EFD. |
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imesisitiza kuwa matumizi ya mashine za kukokotoa kodi za kielektroniki (EFDs), ni sahihi na kila mfanyabiashara anapaswa kuwa nayo.
Kaimu Kamishina wa TRA, Rished Bade, alisema hayo jana jijini hapa alipozungumza na waandishi wa habari.
Wakati kukiwa na mgomo nchi nzima dhidi ya matumizi ya mashine hizo, Bade alisisitiza kuwa wakati wa kufanya biashara bila ya kulipa kodi halali umepitwa na wakati na kila mmoja anapaswa kulipa kodi kutokana na kile alichouza na si vinginevyo.
Mbele ya Kamishina wa Kodi ya Ndani, Patric Kayombo na Meneja wa TRA, Mkoa wa Arusha, Evarest Kileva, Bade alisema serikali kabla ya kuanza mfumo huo mpya mwaka 2010, ilitoa elimu nchi nzima.
Alisema Serikali haijatoza kodi mpya na kamwe haiwezi kumtoza mfanyabiashara yeyote kodi kubwa wala ndogo bila sababu za msingi.
Alisisitiza kuwa kodi inayotokana na mashine hizo ni kodi halali ambayo mfanyabiashara amefanya mauzo yake baada ya kuuza bidhaa iliyokuwa dukani, kodi hiyo inayorekodiwa na mashine hizo ndiyo inayopaswa kulipiwa kodi.
"Kuna baadhi ya wafanyabiashara wanapotosha ukweli juu ya utumiaji mashine hizi …wanataka kutumia mgomo kujinufaisha kwa kuwa mashine hizi rekodi yake inaonesha wazi bila kificho, sehemu zote ikiwamo TRA,’’ alisema.
Alisema mashine zinazosambazwa nchini kupitia kampuni 11 zilizopewa kazi hiyo, zimetengenezwa kwa maelekezo ya uhalisia wa matumizi ya kitanzania na risiti zake zikitolewa katika maduka ya wafanyabiashara kumbukumbu hizo huoneshwa TRA.
Kuhusu mgomo, alisema sheria iko wazi na hatua kali zitachukuliwa dhidi ya wafanyabiashara wasio waaminifu.
"Hakuna kodi mpya iliyoletwa katika mashine hizo bali ni kutaka kila mfanyabiashara auze bidhaa zake na kulipa kodi kutokana na alichouza kihalali bila kificho,’’ alisisitiza.
Kamishna Bade alisema awali kulikuwa na changamoto katika suala hilo, lakini walikaa pande zote na kujadili na kupata ufumbuzi lakini anasikitika kuona baadhi ya wafanyabiashara na TCCIA wanaacha kusema ukweli na kudiriki kupotosha umma juu ya ukweli wa mashine hizo.
Baadhi ya mikoa nchini juzi na jana, ilikumbwa na mgomo wa wafanyabiashara kufunga maduka yao kushinikiza kuondolewa kwa matumizi ya mashine hizo, na matokeo yake ni kusababisha usumbufu kwa wateja.

No comments:
Post a Comment