Simon Msuva wa Yanga akikwatuliwa na beki wa Komorozine. |
Matokeo hayo yamekuja baada ya ushindi wa mabao 5-2 walioupata vijana hao wa Jangwani katika mchezo uliochezwa mjini Moroni jana usiku.
Yanga sasa imefanikiwa kutinga raundi ya pili ya michuano hiyo baada ya kuiondosha mashindanoni timu hiyo kutoka Visiwa vya Comoro kwa jumla ya mabao 12-2, kufuatia ushindi wa mabao 7-0 walioupata jijini Dar es Salaam wiki iliyopita.
Kwa kutinga hatua hiyo, Yanga sasa itakabiliana na timu ya National Al Ahly ya Misri kwenye raundi ya pili ya michuano hiyo ambapo mchezo wa kwanza unatarajiwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Taifam jijini Dar es Salaam.
Katika mechi ya jana, mabao ya Yanga yalifungwa na Mrisho Ngassa aliyeweka wavuni mabao matatu, huku Hamis Kiiza na Simon Msuva wakifunga bao moja moja.
Mpaka sasa, Ngassa ameshafanikiwa kufunga mabao sita katika mechi mbili kwani kwenye mechi ya kwanza alifunga pia mabao matatu.
No comments:
Post a Comment