Halmashauri ya Kinondoni imekumbwa na kashfa ya matumizi mabaya ya fedha baada ya kubainika imedanganya kwamba ilitumia Sh milioni 20 kukarabati na kupanua mochari ya Hospitalini ya Mwananyamala wakati siyo kweli.
Inadaiwa ilidanganya kupitia taarifa zake, ikionesha imetumia Sh milioni 20 kukarabati na kupanua mochari ya Hospitali ya Mwananyamala ili ihifadhi miili 50 badala ya 15 wakati kilichobainika kufanyika ni ujenzi wa korido kutoka wodini hadi mochari.
Katika nyaraka za mpango wa halmashauri hiyo kwa mwaka 2011/2012, zilionesha mochari hiyo iliboreshwa kwa kiasi hicho cha fedha huku nyaraka ya ripoti ya utekelezaji zikionesha upanuzi huo umefanyika kwa asilimia 100 kwa sh milioni 31.
Hata hivyo ripoti ya Kamati ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii (SAM) , imebaini kutokuwepo utekelezaji huo jambo ambalo lilishangaza wadau waliokutana jana Dar es Salaam katika uwasilishaji wa mrejesho huo. Mchakato huo wa ufuatiliaji wa uwajibikaji unasimamiwa na taasisi ya Sikika.
Mkutano huo ulihusisha madiwani, maofisa watendaji kata, wenyeviti 20 kutoka kamati za zahanati Kinondoni, asasi mbalimbali na makundi mengine kutoka halmashauri ya Kinondoni.
Licha ya kuwepo taarifa nyingine, suala la Mwanaymala lilionekana kushangaza wengi huku Katibu Tawala wa Wilaya ya Kinondoni, Celestine Onelit akisisitiza kwamba taarifa hizo hazina budi kuripotiwa kama zilivyo, kama njia ya kujiboresha zaidi.
Akiwasilisha ripoti ya usimamizi wa utendaji, Mjumbe kutoka SAM, Samwel Mhando alisema ripoti ya utekelezaji inaonesha kuwepo kwa upanuzi wa mochari ili ichukue miili 50 kwa siku badala ya 15 lakini hakuna upanuzi wowote uliofanyika wakati fedha inaonekana ilitumika.
Akichangia mada, Mwenyekiti wa SAM, Alexander Mwidima alisema wakati wakiwa hospitali ya Mwananyamala, Mganga Mkuu wa hospitali hiyo, alisema kilichojengwa katika hospitali hiyo ni korido la kutoka wodini hadi eneo la mochari . Kwa mujibu wa Mwidima, Mganga Mkuu wa Mwananyamala alithibitisha kwamba hafahamu zaidi kuhusu ukarabati wa mochari.
“Kabla ya kuanza kazi ya utafiti tulionana na Mkurugenzi wa Kinondoni ambaye ndiye aliyetupatia nyaraka hizo ambazo kamati ilisoma na kuanza kuzunguka katika vituo vya afya kuona hali ikoje…tukiwa hapo Mwananyalama tulimhoji mhandisi aliyejenga korido hiyo kilichofanyika hapo ambapo pia Mganga mkuu alisisitiza kilichojengwa ni korido,” alisema Mwidima.
Katibu Tawala wa Wilaya, Onelit ambaye alifika katika mkutano huo kwa ajili ya ufunguzi, alitaka wanakamati ya SAM kusema waliyoona bila kuficha akisema ndivyo hali halisi ilivyo na kwamba hiyo ndiyo njia ya kujirebisha.
Awali alisema SAM bado wana nafasi ya kuishauri serikali ili huduma za afya zitolewe kama inavyopangwa.

1 comment:
Funga hao wote waliokula pesa zetu wezi wakubwa hao
Post a Comment