![]() |
| William Mgimwa. |
Rais Jakaya Kikwete amemtembelea Waziri wa Fedha, William Mgimwa katika Hospitali ya Kloof mjini Pretoria, Afrika Kusini, ambako Waziri huyo amelazwa akitibiwa.
Rais Kikwete ambaye alikuwa katika ziara ya kikazi ya siku tatu nchini Afrika Kusini, alimtembelea Waziri Mgimwa jioni ya Jumanne wiki hii, baada ya kumaliza kushiriki Kumbukumbu ya Kifo cha aliyekuwa kiongozi mashuhuri wa Afrika Kusini, Mzee Nelson Mandela.
Katika mazungumzo yaliyochukua robo saa, Waziri Mgimwa alimwambia Rais Kikwete: “Hali yangu inaendelea vizuri Mheshimiwa Rais na nakushukuru kwa kupata muda wa kuja kuniona. Inatia moyo na nguvu sana Mheshimiwa Rais.”
Naye Rais Kikwete alimtakia heri Waziri Mgimwa ambaye amekuwa kwenye hospitali hiyo kwa muda sasa na baadaye alipata nafasi ya kusalimiana na wana-familia ikiwa ni pamoja na mke wake na binti yake mkubwa.
Wakati huo huo, Rais Kikwete juzi alimtembelea Ofisa Mwandamizi wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, Jenerali Vicent Mritaba ambaye amelazwa kwenye Hospitali ya Mifupa ya Lynnmed Clinic iliyoko eneo la Lynnwood mjini Pretoria.
Rais Kikwete amemtembelea Jenerali Mritaba akiwa njiani kwenda Uwanja wa Ndege wa Kituo cha Jeshi la Anga la Waterkloof, kupanda ndege kurejea nyumbani.
Kabla ya kuondoka nchini, Rais Kikwete alikuwa miongoni mwa viongozi 91 wakuu wa Serikali na nchi waliotoa heshima za mwisho kwa mwili wa Mzee Mandela na kutia saini Kitabu cha Kumbukumbu cha kifo cha kiongozi huyo.
Viongozi hao walikuwa wa kwanza kutoa heshima zao za mwisho kwa mwili huo ambao utalazwa kwenye Ofisi ya Urais wa Afrika Kusini zilizoko katika majengo ya Union Buildings, Pretoria.

No comments:
Post a Comment