Mkalimani aliyekuwa akitafsiri kwa alama kwa ajili ya walemavu wasiosikia yaliyokuwa yakisemwa na viongozi na watu mbalimbali katika mazishi ya kitaifa ya kiongozi wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela katika uwanja wa FNB, Johannesburg, Jumanne alipatwa na uchizi jukwaani.
Thamsanga Jantjie (34) amesema ana sifa za kazi hiyo, lakini siku hiyo alianza kusikia sauti ngeni kichwani mwake na njozi, matokeo yake alama alizokuwa akizitumia zilipoteza maana halisi kwa walengwa.
Jantjie jana aliomba radhi na kusema hakujua kilichosababisha kupatwa na hali hiyo, na kusema hata hivyo alipata dawa.
Akizungumza nyumbani kwake mjini Bramfischerville, juzi, alisema anafanya kazi na kampuni inayoitwa SA Interpreters ambayo ilikodiwa na chama tawala cha ANC, kwa ajili ya shughuli hiyo. Alisema alilipwa dola 85.
Jantjie aliliambia gazeti la Star la Johannesburg: “Nisingeweza kufanya chochote wakati huo. Nilikuwa peke yangu pale katika hali ngumu na ya hatari. Nilijaribu kujidhibiti ili nisiioneshe dunia kilichokuwa kikiendelea. Nasikitika sana. Ni hali niliyojikuta nayo bila kutarajia.”
Aliliambia gazeti hilo, kwamba amekuwa akipata dawa kutokana na uchizi huo, ambao umemfanya aishi kwa kutegemea msaada wa kijamii. Alisema kazi hiyo ndiyo inamfanya aweze kuishi.
Hakutaka kuzungumzia madai kutoka kwa wataalamu wa lugha, kwamba alidanganya tafsiri yake katika sherehe hizo zilizohudhuriwa na viongozi wengi wa kimataifa na zilizorushwa moja kwa moja duniani.
Chama cha Wasiosikia cha Afrika Kusini jana kilidai kuwa alikuwa mkalimani bandia na kusema alikuwa akibuni alama. “Alikuwa akirusharusha mikono tu,” madai yalisema.
Akihojiwa na kituo cha redio, Jantjie alisema kinachomfurahisha kwa kazi yake ni kwa kuwa sherehe hizo zilimhusu shujaa wa mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi, ambaye alifariki dunia wiki moja iliyopita akiwa na umri wa miaka 95.
Alikiambia kipindi cha Talk Radio 702: “Bila shaka, bila shaka. Nadhani mimi ni bingwa wa lugha za alama.” Kwa mujibu wa gazeti la The Sun, watumiaji wa mtandao wa twitter wanaotumia lugha ya alama wanadai mkalimani huyo alikuwa mara kwa mara akitumia alama ya ‘punda’ na ‘samaki aina ya kamba’.
Mtandao wa Eye Witness News nao uliripoti kwamba wakufunzi wa lugha za alama walisema pia alikuwa akitumia alama za ‘farasi’.
Mlemavu wa kusikia wa Afrika Kusini, Braam Jordaan ambaye pia ni mjumbe wa Bodi ya Shirikisho la Wasiosikia la Dunia, alisema anaamini mkalimani huyo alikuwa akijirekebisha kadri muda ulipokuwa ukisonga mbele.
Serikali, ambayo ndiye msimamizi wa sherehe hizo, ilisema haikuwa inamtambua mkalimani huyo. Hali kadhalika ANC nayo ilikanusha kujua nini kilikuwa kikiendelea jukwaani ingawa katika matukio makubwa ya chama hicho mwaka jana, yalimwonesha mkalimani huyo akifanya ukalimani kwa wasiosikia akiwa jukwaani karibu na Rais Jacob Zuma.
Katika hatua nyingine, wakati akishiriki maombi maalumu ya Mandela katika uwanja huo Jumanne mpambanaji mwingine dhidi ya ubaguzi wa rangi Askofu Mkuu mstaafu Desmond Tutu ameibiwa nyumbani kwake.
Wezi walilenga nyumba yake katika kitongoji anachoishi jijini Cape Town, wakijua kuwa kiongozi huyo wa kiroho alikuwa umbali wa zaidi ya kilometa 800 akishiriki sherehe za mazishi ya kitaifa ya Mandela.
Hii ni mara ya pili katika kipindi cha miezi minne Askofu Mkuu huyo wa zamani wa Cape Town kuvamiwa na majambazi.
“Naweza kuthibitisha, kwamba usiku wa jana (juzi) kulikuwa na tukio la ujambazi,” msaidizi wake, Roger Friedman alisema jana.
“Hatuwezi kwa sasa kusema kwa uhakika ni nini kimeibwa, Askofu Mkuu na mkewe hawapo nyumbani. Nyumba haikutekwa.” Polisi ilisema katika taarifa yake, kwamba uhalifu huo ulifanyika Jumanne kati ya saa 1 na 3 usiku.
“Kwa sasa hatuwezi kutoa maelezo zaidi, kwa kuwa uchunguzi kuhusu tukio hilo bado unaendelea,” msemaji wa Polisi alisema. “Hakuna mtu aliyekwishakamatwa kuhusu tukio hilo.”
Maofisa wa Polisi hawakuwa tayari kuthibitisha kama kuna kitu kilichoibwa nyumbani kwa mshindi huyo wa Tuzo ya Nobel mwaka 1984.
Katika wizi wa kwanza Agosti 7 wezi walivunja nyumba hiyo wakati Askofu Mkuu huyo na mkewe Leah, wakiwa wamelala na kuchukua vitu vidogo vidogo.
Ujambazi ni matukio ya kawaida Afrika Kusini, kutokana na ukosefu wa usawa na kuwa na Serikali dhaifu. Tutu (82), alitoa maombi ya kufungia sherehe za juzi katika uwanja wa Soccer City.
Aliwataka Waafrika Kusini kufuata mfano wa Mandela akisema: “Nataka kuuonesha ulimwengu, kwamba tunaweza kujitokeza hapa na kusherehekea maisha ya mtu mashuhuri.”
Sherehe hizo pia zilisindikizwa na hotuba iliyokubalika ya Rais wa Marekani, Barack Obama, na salamu za pole kutoka kwa viongozi wa dunia ambao walimsifu Mandela kama mmoja wa viongozi mashuhuri wa karne ya 20.
Hata hivyo, habari kwamba Tutu aliibiwa wakati huo, ni moja ya taarifa nyingi za matukio kama hayo yaliyohusiana na siku hiyo.

No comments:
Post a Comment