Habari zilizotufikia hivi punde zinasema kwamba ndege ya Shirika la ndege la Precision Air imepata ajali wakati ikijaribu kutua kwenye uwanja wa ndege wa Arusha muda mfupi uliopita.
Ajali hiyo imetokea baada ya ndege hiyo aina ya ATR kupasuka magurudumu yake yote manne ya nyuma wakati ikijaribu kutua uwanjani hapo.
Ndege hiyo ilikuwa imebeba abiria kadhaa akiwemo Waziri Mkuu mstaafu na mbunge wa Monduli, Mhe. Edward Lowassa ambao wote wamenusurika kifo
Tukio hilo lilisababisha taharuki kubwa miongoni mwa abiria waliokuwamo kwenye ndege hiyo.
"Yaani Mungu ni mkubwa kwa kweli, ametunusuru maisha yetu na kiongozi kipenzi chetu Lowassa... Mungu atamlinda jamani... siamini", alisikika akisema mama mmoja wa abiria hao.

No comments:
Post a Comment