![]() |
| Wilfred Lwakatare akisindikizwa kutoka mahakamani. |
Upelelezi wa kesi ya kula njama ya kudhuru kwa sumu, inayomkabili Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilfred Lwakatare na mwenzake, Ludovick Joseph haujakamilika.
Wakili wa Serikali, Flora Massawe alidai hayo jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakati kesi hiyo ilipotajwa.
Hakimu Mkazi Aloyce Katemana aliahirisha kesi hiyo hadi Januari 9, mwakani kesi hiyo itakapotajwa tena na washitakiwa hao wataendelea kuwa nje kwa dhamana.
Awali, Lwakatare na Joseph, walikuwa wakikabiliwa na mashitaka ya ugaidi katika Mahakama hiyo, mashitaka ambayo yalikuwa hayana dhamana.
Mei 8, mwaka huu, Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam iliwafutia mashitaka hayo na kubaki na shitaka hilo la jinai linalodhaminika.
Washitakiwa walipata dhamana baada ya kutimiza masharti yaliyowataka kuwa na wadhamaini wawili waliosaini hati ya Sh milioni 10, waliwasilisha hati zao za kusafiria na hawatatakiwa kusafiri nje ya Mkoa bila kuwa na kibali cha Mahakama.
Washitakiwa hao wanadaiwa kuwa Desemba 28, mwaka jana katika eneo la King’ongo, Kinondoni, Dar es Salaam walipanga njama ya kutenda kosa la jinai la kutumia sumu kumdhuru Mhariri wa gazeti la Mwananchi, Dennis Msacky.

No comments:
Post a Comment