Anna Abdallah. |
Harakati
za kupata rais mwanamke zimeanza baada ya ulingo wa wanawake kutangaza kufanya
ushawishi kwenye vyama vyote vya siasa wanawake wenye uwezo wapewe nafasi
kugombea.
Mwenyekiti
wa ulingo wa wanawake, Anna Abdalah amesema ile dhana ya kwamba chama fulani
kina mtu wake, haina nafasi.
Chini
ya ulingo huo, Abadalah amesema wameanza kuzungumza chini chini na wanawake
ndani ya vyama kushawishi wajitokeze kugombea urais siyo tu udiwani na ubunge.
Abdalah
alisema hayo kwenye mahojiano jana na TBC 1 kwenye kipindi cha jambo juu ya
ulingo wa wanawake na katiba.
Alipohojiwa
kama harakati hizo ameanza kuzifanya katika CCM ambacho ni chama chake, alisema
ameanza muda mrefu.
Ulingo
huo unaohusisha wanawake wote nchini bila kujali itikadi zao, unaendelea kudai
wanawake kuwa sehemu ya uongozi wa juu
katika vyama vya siasa.
Kwa
mujibu wa Anna Abdallah, TLP pekee ndicho chama chenye nafasi ya juu ya uongozi
inayoshikiliwa na mwanamke.
Vyama
vingine vyote vinashutumiwa nafasi za mwenyekiti, makamu na ukatibu mkuu kushikiliwa
na wanaume.
Kutokana
na hali hyo, mwanasiasa huyo mkongwe, Abdallah amesema kwa kuwa wanawake walio
wengi ndio wapiga kura waaminifu, harakati zilizoanza zitashawishi kuhakikisha
wanawake wanachaguliwa katika nafasi za juu kwenye vyama.
Hata
hivyo alipongeza serikali kwa kujitahidi kuzingatia usawa wa kijinsia kwenye
uteuzi nafasi mbalimbali.
No comments:
Post a Comment