HATIMAYE NDEGE YA ETHIOPIA YANASULIWA KWENYE TOPE ARUSHA...


Hapa ndipo iliponasa ndege hiyo.

Hatimaye  ndege  kubwa aina ya Boeing 767 mali ya Shirika la Ndege la Ethiopia, iliyotua kwa dharura juzi, uwanja wa ndege wa Arusha ikiwa na abiria 213, imenasuliwa kutoka kwenye  tope na kuwekwa kwenye lami.

Kazi ya kuvuta ndege hiyo  ilianza saa 8.10  mchana na kufanikiwa kugusa matairi yake kwenye lami ya uwanja saa 9:02 mchana.
Ndege hiyo ilivutwa na gari namba T.897 APE mali ya kampuni ya Flying Cargo ya Arusha na gari namba T. 958 AKS mali ya kampuni ya Simba Trucking.
Ndege hiyo ilikuwa inatoka nchini Addis Ababa na ilikuwa itue Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) ikiwa na abiria 213, ilikaguliwa na wakaguzi sita  wa ndege kutoka Ethiopia na wakaguzi  wawili  wa Tanzania na kuona haina shida hivyo kuamuru ivutwe.
Kwa mujibu wa Ofisa Uendeshaji wa Uwanja wa  Mdogo wa Arusha, Roland Mwalyambi  akizungumzia kuhusu kuruka kwa ndege hiyo alisisistiza kuwa ingawa si msemaji lakini wataalamu watatoa taarifa za kitaalam kama ndege hiyo
Itawezaje kuruka kutoka katika kiwanja hicho kidogo chenye njia ya kukimbilia ya kilomita 1.6 .

No comments: