Matairi mawili kati ya manne ya ndege hiyo yaliyopasuka wakati ikitua. |
Abiria kadhaa akiwemo Waziri Mkuu wa zamani ambaye kwa sasa ni Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, wamenusurika kufa baada ya ndege waliyokuwa wakisafiria kupasuka matairi yote manne ya nyuma wakati ilipokuwa ikitua katika Uwanja wa Ndege wa Arusha uliopo eneo la Kisonga, jana mchana.
Ndege hiyo ya shirika la ndege la Precision aina ya ATR yenye namba PW 0422 ilipata ajali hiyo wakati ikitua.
Kutokea kwa ajali hiyo kumethibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas aliyesema ndege hiyo ilikuwa ikitokea Dar es Salaam kwenda Arusha.
Kamanda Sabas alisema ajali hiyo ilitokea majira ya saa 7 mchana baada ya matairi yake manne ya nyuma kupasuka wakati ikitua katika uwanja mdogo wa ndege wa Kilimo Anga Arusha.
“Ajali imetokea majira ya saa saba mchana lakini hakuna mtu yeyote aliyepoteza maisha wala kujeruhiwa katika ajali hiyo kwa kuwa ilitua salama,” alisema.
Alisema mpaka hivi sasa ndege hiyo ipo katika uwanja huo huku wataalamu mbalimbali wakiendelea na uchunguzi wa tukio hilo ili kubaini sababu ya ndege hiyo kupasuka magurudumu yake yote manne ya nyuma.
Hata hivyo, Kamanda Sabas alisema uchunguzi wa awali unaonesha kuwa huenda sababu kubwa ya kupasuka kwa magurudumu hayo ni kutokana na matope yaliyokuwepo katika njia ya kukimbilia ndege kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha mkoani hapa.
Alisema kwa taarifa hizo za awali alizonazo, hakuweza kupata namba ya ndege hiyo iliyopata ajali wala idadi ya abiria wake kwa kuwa alikuwa nje ya ofisi yake na kuahidi kuitolea ufafanuzi zaidi atakaporejea ofisini.
Wakati hayo yakitokea Arusha, imeripotiwa kwamba majeruhi 35 kati ya 93 walionusurika kifo katika ajali ya basi la Kampuni ya Burudani linalosafiri kati ya Korogwe na Dar es Salaam, wameruhusiwa kurudi nyumbani baada ya kupatiwa matibabu na hali ya afya zao kuonekana inaendelea vizuri.
Majeruhi hao ni wale waliopokelewa juzi kwenye Hospitali ya Magunga iliyoko wilayani Korogwe kutoka kijiji cha Kwalaguru kilichopo wilayani Handeni eneo ilikotokea ajali hiyo iliyosababisha abiria wengine 12 kupoteza maisha papo hapo akiwemo dereva wa basi hilo, Luta Mpenda.
Miili ya marehemu hao iliyokuwa imehifadhiwa katika chumba cha maiti cha hospitali ya Magunga hadi jana mchana tayari ilikuwa imetambuliwa na kuchukuliwa na familia zao kwa ajili ya shughuli za maziko zilizofanyika katika maeneo tofauti ya wilaya hiyo ya Korogwe.
Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Magunga, Dk Aedes John amethibitisha kuruhusiwa kwa majeruhi hao alipozungumza katika mahojiano na wanahabari hospitalini hapo jana mchana.
Alisema majeruhi wengine 15 wamelazimika kuwahamishia katika Hospitali za Rufaa za Bombo (Tanga), KCMC (Moshi) na Taasisi ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu ya Muhimbili (MOI) kutokana na kupata majeraha makubwa yaliyosababishwa
na kuvunjika kwa viungo ikiwemo miguu, mikono na kifua pamoja na kuvuja damu kwa wingi.
“Kati ya majeruhi hao tuliowapa rufaa yumo mtoto mdogo mmoja, wanawake wanne pamoja na wanaume 10 na kwamba kati yao waliopelekwa MOI ni watano, hospitali ya Bombo mmoja, majeruhi kumi walihamishiwa KCMC,” alisema.
Aidha, alibainisha kwamba kuhusu majeruhi wengine waliosalia akiwemo mtoto mmoja wanawake 15 pamoja na wanaume tisa ambao bado wamelazwa katika hospitali hiyo ya Magunga hali ya afya zao imeendelea kuimarika.
Katika hatua nyingine, baadhi ya wakazi wa Mkoani Tanga waliozungumzia kwa nyakati tofauti tukio la ajali hiyo walimtaka Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga, Costantine Massawe kuwawajibisha askari wa usalama barabarani waliokuwa zamu jana katika vituo vya ukaguzi vya askari barabarani vilivyopo kati ya Korogwe na eneo la ajali, kwani waliruhusu basi hilo kuendelea na safari licha ya kujaza abiria kupitia kiasi.

No comments:
Post a Comment