Susan Kaganda. |
Siku moja baada ya ajali ya basi la Burudani mkoani Tanga, basi jingine la Simiyu Express limeua abiria wawili na kujeruhi wengine 14 baada ya basi hilo kupinduka katika eneo la Ihumwa nje kidogo ya Manispaa ya Dodoma.
Basi hilo lenye namba za usajili T 717 ANL aina ya Scania lilikuwa likiendeshwa na dereva aliyetambulika kwa jina la Mramba Issa (31).
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani hapa Susan Kaganda, alisema kuwa basi hilo lilikuwa linatokea Bariadi kwenda Dar es Salaam likiwa na abiria 60 liliacha njia na kupinduka kutokana na mwendo kasi. Kamanda alisema kwamba ajali hiyo ilitokea jana alfajiri majira ya saa tisa katika barabara ya Dodoma-Dar es Salaam eneo la Elshadai.
Kamanda Kaganda aliwataja waliofariki katika ajali hiyo kuwa ni pamoja na dereva wa basi hilo Mramba Issa mkazi wa Magomeni, Dar es Salaam na Flora Ernest (21) Mwalimu wa shule ya msingi Mwamoto Kolokolo, Bariadi.
Aidha kamanda akizungumzia zaidi ajali hiyo alisema kwamba basi hilo lilikuwa likiwakwepa askari wa barabarani kwa kupita njia za panya. Alifafanua kuwa kwa basi hilo kusafiri usiku huo ni kukwepa askari.
Aliwataka pia wamiliki wa magari kuweka madereva wawili kwa magari ya masafa marefu na pia wazingatie sheria za barabarani.

No comments:
Post a Comment